Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani wamesema wana uhakika kuwa uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa wa amani na haki kwa kila mmoja anayeshiriki uchaguzi huo, wakiamini kuwa siku ya Oktoba 29, 2025 kutakuwa na amani na utulivu pia kutokana na uthibitisho na uhakika walioupata kwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyesema kuwa serikali na Vyombo vya Dola vimejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kupiga kura katika mazingira salama na tulivu kote nchini.
Wananchi hao akiwemo Bi. Mwinyimvua Kasosoma na Mwanaidi Stephano, wakazi wa Kwa Mathias, Kibaha Mkoani Pwani wamesema hayo leo Oktoba 15, 2025 wakati wakizungumza na mwandishi wetu na kusisitiza kuwa wao na familia zao watajitokeza wote wenye sifa kwenda kupiga kura na kumchagua Kiongozi wanayeamini atawaletea maendeleo.
Aidha wamekumbusha umuhimu wa kuheshimu sheria na Miongozo yote ya Uchaguzi Mkuu, wakisema mara baada ya Kupiga kura ni muhimu kila mmoja kuondoka kwenye Vituo vya kupigia kura na kwenda kuendelea na shughuli nyingine za kiuchumi, wakijitenga na baadhi ya maneno ya wanasiasa wanaowataka wafuasi wao kusalia vituoni ili kuhakikisha ulinzi wa kura ama kuachana na upigaji wa kura na kuandamana ili kuitika hamasa ya baadhi ya wanaharakati na wanasiasa.
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unafanyika Oktoba 29, 2025 ambapo Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari amewahakikishia wananchi wote usalama na utulivu wa kutosha siku hiyo, akionya wale wote wanaopanga kufanya vitendo vya uhalifu ama uvunjifu wa amani nchini.
1 Comments
Ushuhuda Wangu Wa Dhati 💖
ReplyDeleteBaada ya baba yangu mdogo kuniacha kwa miezi saba ndefu, nilivunjika kabisa. Alinifungia kwenye mitandao yote ya kijamii, akasafiri mbali, na hakukuwa na njia ya kumfikia. Nilikaribia kukata tamaa juu yetu, lakini ndani kabisa nilijua singeweza kupata mtu yeyote ambaye angenipenda na kunitendea jinsi alivyonitenda.
Siku moja, bosi wangu kazini aliona jinsi nilivyokuwa na huzuni na akanitambulisha kwa Dk. Dk. Dawn alisikiliza hadithi yangu na akaahidi kwamba mpenzi wangu atanirudia ndani ya siku tatu. Kusema kweli, sikuamini mwanzoni—lakini kwa mshangao mkubwa zaidi, siku ya tatu simu yangu iliita. Ilikuwa ni yeye! Alikuwa akilia na kuomba msamaha, akisema hataniacha tena.
Tangu siku hiyo, uhusiano wetu umekuwa wenye nguvu na mzuri zaidi kuliko hapo awali. Amekuwa akinipenda na kunijali sana mimi na mtoto wetu, na sasa tunafunga ndoa baada ya miezi miwili tu! ❤️
Shukrani zote kwa Dk. Dawn, ambaye kwa kweli aliwezesha jambo lisilowezekana. Ninampendekeza kwa moyo wote kwa yeyote anayekabiliwa na changamoto katika:
Masuala ya mahusiano au ndoa
Ugonjwa au magonjwa
Ugumba au matatizo ya bahati nasibu
Kesi za mahakama au kurejesha mali
Dk. Dawn kweli hutatua matatizo kwa ufanisi na hurejesha furaha katika maisha ya watu.
Wasiliana na Dr. Dawn kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com