Header Ads Widget

DKT MWINYI AAHIDI KUWEKA KITUO MAALUM UTOAJI WA HUDUMA ZA KITABIBU KWA WATU WENYE ULEMAVU

 

Na mwandishi wetu

Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kuanzisha Kituo Maalum cha utoaji wa huduma za kitabibu kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuhakikisha kundi hilo linapata huduma bora za afya na haki sawa katika jamii.

Akizungumza katika mkutano wake wa kukutana na kundi la watu wenye ulemavu Zanzibar, ikiwa ni muendelezo ya mikutano yake ya kampeni, Dkt. Mwinyi amesema Serikali atakayoiongoza itaweka mazingira rafiki yatakayowawezesha watu wenye ulemavu kupata matibabu stahiki bila vikwazo vya kifedha au ubaguzi.


Vilevile, ameeleza kuwa Serikali itahakikisha inaongeza nafasi za ajira na uteuzi kwa watu wenye ulemavu, ili nao wawe sehemu ya maamuzi na maendeleo ya Taifa.

Amesema pamoja na hatua hizo serikali yake itaendelea kuimarisha ustawi wa watu wenye ulemavu kiuchumi kwa kuendeleza kutoa mikopo isiyokua na riba pamoja na uwezeshaji wa mitaji ili kuendesha shughuli zao za kiuchumi 


Kwa mujibu wa Dkt. Mwinyi, sera hizo ni sehemu ya mpango mpana wa kuimarisha ustawi wa jamii, kupunguza ubaguzi na kujenga Zanzibar inayompa kila mtu nafasi ya kufikia ndoto zake bila kikwazo cha hali yake ya kimwili.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI