Header Ads Widget

KATIBU MKUU WA BARAZA LA MAWAZIRI ZAMBIA APONGEZA HUDUMA ZA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA


Diplomasia ya kiuchumi na sekta ya utalii wa matibabu (Medical Tourism) katika ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC) umezidi kuimarika. Hii ni kufuatia ziara ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri nchini Zambia, Ndugu Patrick Kangwa, alipotembelea banda la Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Taasisi ya Mifupa na Ubongo MOI ililopo chini ya Banda la Tanzania katika Maonyesho ya 98 ya Kilimo na Biashara yanayoendelea jijini Lusaka. 

Ndugu Kangwa amepongeza namna hospitali inavyotekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu inayosema "Fostering Trade and Investment" (Kukuza Biashara na Uwekezaji). 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Ndugu Kangwa alieleza kuvutiwa kwake na ubora wa huduma za kibingwa zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ikiwemo matibabu ya magonjwa ya moyo, mifupa, upasuaji wa mgongo, pamoja na huduma za kibingwa za uzazi na utatuzi wa changamoto za kushika ujauzito. 

Alibainisha kuwa uwezo huo mkubwa wa kitabibu ni fursa adhimu kwa raia wa Zambia na nchi jirani kupata matibabu ya uhakika bila kusafiri umbali mrefu. Mbali na viongozi wa kitaifa, banda la MZRH limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa raia na wadau wa afya nchini Zambia waliomiminika kujionea, kujifunza, na kupata ushauri wa kitaalamu.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI