Na Mwandishi wetu, Mtwara
Watafiti wa zao la karanga Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele wamehamasisha wakulima wa zao hilo kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na kituo hicho ambazo zitaongeza tija kwa kulima na kupata mazao mengi shambani.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akiongea na waandishi wa habari Mratibu wa zao la Karanga kitaifa kutoka Tari Naliendele Dr Happy Daudi watanzania wanapaswa waamke walime karanga kwa wingi kwakuwa sasa zipo mbegu zenye matokeo chanya.
Alisema kuwa mpaka sasa wanazo mbegu aina 11 ambazo zina faa kulimwa katika maeneo mengi ya nchi ambapo mafunzo mbalimbali yameshaanza kutolewa na kitengo hicho ili kuhakikisha kila mtanzania anaetaka kulima karanga anapata utalaam na mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na taasisi hiyo.
“Unapopanda mbegu bora shamba unatakiwa upate 10 hii ndio inaongeza mavuno kwa mkulima wa karanga ndio maana tunahamasiha mkulima atumie mbegu hizi alime eneo dogo lakini apate mavuno mengi yenye tija” alisema Dr Daudi
Mtafiti msaidizi wa zao la karanga kutoka Tari kituo cha Naliendele Anthony Bujiku ambapo alisema ni vema wakulima wakatambua sifa za mbegu hizo na kuzitumia kwa wingi ili kuleta hamasa ya kulima zao hilo muhimu kibiashara.
“Uzuri wa hizi mbegu zina stahimili ukame na pia hazishambuliwi na magonjwa ndio maana tunahamasisha wakulima kulima kwa wingi zaidi ili kuongeza uzalijsaji hata katika maonyesho ya sabasaba tulipeleka elimu hii pia ili kuongeza hamasa ya watanzania kulima zao la karanga”
Tunayo mazao yanayotoa mafuta ikiwemo ufuta na karanga tukilima kwa ufasaha kwakufuata kanuni bora za kilimo na tukafuata ushauri wa watalaamu wetu naimani teknologia hii inaweza kuzaa matunda kwa kasi kubwa”
MWISHO
0 Comments