Na Hamida Ramadhan Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga amesema Serikali inawekeza miradi mingi lakini haidumu kwa kuwa wananchi wengi hawana mwamko wa maendeleo kutokana na dhana ya umaskini inayowakabili.
Anna ameyasema hayo leo Jijini hapa kwenye mjadala kuhusu nini mchango wa Asasi za kiraia kwa jamii pamoja na utoaji mchango wa Msaada wa kisheria kwa jamii katika wiki ya AZAKI inayoendelea Jijini Dodoma.
Aidha amesema ,wananchi wanatakiwa kuwa na uwezo wa kutambua thamani ya miradi ili waweze kuitunza na kuiendeleza miradi hiyo
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa wananchi wanatakiwa kuelimishwa kuhusu maana ya Maendeleo na umuhimu wake ili waweze kushiriki ujenzi wa Maendeleo kwa vitendo.
"Ni ukweli usiopingika umaskini usipo tibiwa itaendelea kuwa kidonda Kwa jamii ambapo karibu asilimia 50 ya watoto waishio mitaani wanatokana na ndoa zilizovunjika Kutokana na ugumu wa maisha,"
Na kuongeza "Tunataka kupambana na umaskini uliopitiliza,tunasaidia jamii msaada wa kisheria pale wanapokuwa wamekwama na wakati mwingine kukosa uwezo wa kumpata wakili Kwa kukosa fedha,hivyo ndivyo tunapambana walau kuiokoa jamii," Anna
Kwa upande wake Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga amezitaka Asasi za Kiraia(AZAKI) kutimiza majukumu yake kwa kuongeza mchango wa maendeleo ya nchi kwa kuweka mizania ya maendeleo kwa mtu mmoja mmoja ili kuleta tija na umuhimu wake kwenye jamii.
Amesema AZAKI nyingi zimekuwa zikifanya kazi vizuri lakini hazijafikia malengo walizojiwekea hasa katika kutokomeza umaskini wa mtu mmoja mmoja.
" Umuhimu wa Asasi hizi utaonekana kwenye jamii ikiwa tu zitapambana na kuchochea maendeleo ya watu na siyo vitu kwani tafsiri ya maendeleo inaanza na watu ," Kiwanga
Mwisho.
0 Comments