Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima Media NJOMBE
Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chadema BAWACHA mkoa wa Njombe Veronica Mlonganile na wenzake watangaza kujivua uanachama na kuachana na Chama hicho Leo.
Viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Wanging'ombe Bwana Patrick Njulumi wamesema wameondoka katika Chama hicho kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubezwa kwa sababu walikuwa wanamuunga mkono aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe.
Wamesema pamoja na kuondoka Chadema lakini wataendelea kufanya Siasa na kuwasemea. wananchi changamoto zao
Leah Masasi Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Jimbo la Lupembe anasema anajiondoa Chadema lakini ataendelea kufanya Siasa katika Nyanja nyingine na uvunjifu wa katiba ya Chama hicho ndicho kilichomuondoa.
Aidha Masasi amesema Mwenyekiti Mpya wa Chadema Taifa Tundu Lissu ameshindwa kuvunja makundi na anawakejeli wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Mbowe na hivyo Chadema kimepoteza mwelekeo.
0 Comments