Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. David Silinde amefanya ufunguzi wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa sekondari, ufunguzi huo umefanyika katika Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam DIT Leo Oktoba 25 kwa niaba ya vituo vingine ambavyo mafunzo ya namna hii yanafanyika. Vyuo vingine zaidi ya DIT ni UDOM na MUST
Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo Naibu Waziri Silinde amemshukuru Mwenyekiti wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF Prof. John Mkoma, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam (DIT) Prof. Preksedis Ndomba na watendaji wake kwa kuona umuhimu wa kufadhiri mafunzo haya kwa walimu 650 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na mitano ya Zanzibar
'Kwetu hii ni hatua kubwa nawashukuru kwa namna ya kipekee wakufunzi wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam , Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya na Chuo cha Habari na Mawasiliano na Sayansi Angavu CIV kilichopo chuo kikuu cha UDOM kwa kuandaa na kuratibu mafunzo haya vizuri naomba niwapongeze sana kwa niaba ya serikali kwa kuwezesha mafunzo haya, ni ukweli usiopingika ulimwengu wa leo umetawaliwa na TEHAMA kwahiyo hatua hii mliyochukua itawasaidia sana washiriki wetu kuendana na ulimwengu wa sasa ' Alimalizia Naibu Waziri Silinde
Prof. Preksedis Ndomba, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
Prof. John Mkoma Mwenyekiti wa Bodi UCSAF
Pius Joseph Kaimu Mkurugenzi UCSAF
0 Comments