@HESLBTanzania wamejitetea kwamba kiwango cha chini cha mkopo walichotoa kwa mwanafunzi ni Tsh2,099,500.Hi ni taarifa ya jumla jumla na haina msingi.Hiyo ni fedha ya kujikimu na hutolewa sawa kwa wote.Bodi waseme kiwango cha chini cha Ada walichotoa ni Shiling ngapi?@abdulnondo2 .
Mwaka huu zaidi ya wanafunzi elfu 8 wa mwaka 1 wameomba mkopo na fedha iliyotolewa na serikali ni Tsh. Bil. 570 .Hivyo walichofanya @HESLBTanzania ni kugawa kidogo kidogo kutaka Rais aone kwamba kiwango alichotoa kimetosha na wanafunzi wengi wamepata mkopo mwaka huu @abdulnondo2
@HESLBTanzania wanapaswa kueleza kwa takwimu kiwango cha chini cha fedha ya Ada,fedha ya mafunzo na viandikwa waliyowapa wanafunzi ni shilingi ngapi?.Na ni wanafunzi wangapi wamepewa Ada,fedha ya mafunzo na viandikwa na wangapi wamenyimwa kabisa.Sio kuongea kiujumla @abdulnondo2
Si mara ya kwanza kwa @HESLBTanzania kutoa mkopo wa kiwango kidogo kwa wanafunzi.2016 kuna wanafunzi walipewa hadi elf 5 kama mkopo kwa mwaka.Baada ya wanafunzi kupiga kelele.20/10/2016,saa 2 usiku Waziri Prof.Ndalichako kupitia TBC akaagiza bodi kupanga mikopo upya @abdulnondo2
Unampa fedha ya ada mwanafunzi Tsh. 400,500 hadi Tsh. 256,000 kati ya Ada Tsh. 3,000,000, kati ya 2,000,000 kati ya 1,500,000 ambayo wanafunzi wanapaswa lipa chuoni ili wasajiliwe kuanza masomo. Umemsaidia nini huyu mwanafunzi? .Huu ni mzigo kwa wazazi maskini .@abdulnondo2
BATCH-1 ya wanufaika 37731 iliwekwa wazi pia kwenye PDF umma tukaona.Aliyepewa Tsh.2,750 yupo BATCH 2 tulitarajia Bodi ingetoa PDF-Document ya orodha ya BATCH-2 kwa umma ili tujionee wote mwanafunzi aliyepewa Tsh. 2,750.Ila hadi sasa Bodi haijatoa PDF ya BATCH-2 @abdulnondo2
Aliyepewa Tsh.2,750 aliomba taarifa zake zisiwe wazi,tulitegemea Bodi itoe majina kwa umma tuone ila Bodi hawajatoa PDF ya BATCH-2 kwa umma.Badala yake wametuma taarifa za kiwango cha fedha kwenye akaunti binafsi za wanafunzi (SIPA) ili hizi kasoro umma tusizione. @abdulnondo2
Kiwango cha chini cha fedha ya Ada walichotoa Bodi ya mikopo ni Tsh.400,500 hadi Tsh.256,000 waliopewa kiasi hiki katika Ada ni wanafunzi wengi zaidi ya 90%.Mwanafunzi aliyepewa Tsh2,750 alinyimwa Ada.Tsh.2,750 aliyopewa ni katika fedha ya field na categori nyingine.@abdulnondo2
Serikal ifahamu kwamba fedha iliyotoa kwa @HESLBTanzania Tsh.Bil 570 haitoshi.Fedha ni ndogo idadi ni kubwa hivyo iongeze fedha kwani kuna wanafunzi wenye sifa hawajapata mkopo hata senti,wengine wamepewa kidogo na kunyimwa categori zingine na wengine wamenyimwa ada @abdulnondo2
0 Comments