Header Ads Widget

BREAKING NEWS:KATIBU WA CCM KILOLO AVAMIWA NA WASIOJULIKANA AUAWA

 

TAZAMA FULL VIDEO YA MAUAJI BOFYA LINK HII
Na Matukio Daima media 

Watu Wasiojulikana Wanadaiwa wamemvamia aliyekuwa katibu wa Chama Cha mapinduzi(CCM)wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Christina Kibiki na kumuua kwa kumpiga risasi .

Taarifa ambayo Matukio Daima media tumeipata inadai kuwa watu hao Wasiojulikana wamefanya uvamizi huo usiku wa kuamkia Leo katika Kijiji Cha njia panda ya Tosa wilaya ya Iringa Vijijini nje kidogo na mji wa Iringa ambako alikuwa akiishi.

Kuwa baada ya kumshambulia kwa risasi alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ya Tosamaganga ambako amefariki Dunia.

Matukio Daima media imezungumza kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo John Kiteve amesema tukio Hilo limemgusa sana na amesokitishwa na tukio hilo .

Huku kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi hajaweza kupatikana ili kuthibitisha tukio Hilo Bado Matukio Daima media inaendelea kufuatilia zaidi.


HABARI KAMILI 

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu 
Chumbani kwa marehemu 

Asifiwe Kibiki Majukuu wa marehemu Christina Kibiki akionesha sehemu ambayo Mawili wa marehemu ulitupwa .

Na Matukio Daima media 

Kufuatia tukio la kuuawa kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kilolo, Christina Kibiki na watu nwasiojulikana akiwa nyumbani kwake kitongoji cha Banawano kijiji cha Ugwachanya kata ya Mseke kilichopo katika Halmashashauri ya wilaya ya Iringa.

Matukio Daima Media imefika nyumbani kwake na kuzungumza na baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu, majirani Pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi juu ya tukio hilo.

Asifiwe Kibiki ni mjuku wa marehemu Christina Kibiki amesema bibi yake alivamiwa na kijana ambaye hawakumtambua  kwa jina wakiwa nyumbani kwao majira ya usiku baada ya kumaliza kula chakula cha usiku na kumlawiti kabla ya kumshambulia.
 
“Tulikuwa tume kaa hapa sebleni na dada yangu, baada ya kumaliza kula chakula cha usiku akafika kijana mmoja akagonga mlango, dada alivyomfungulia akamuulizia bibi, dada yangu akasita sijui alikuwa na roho gani na yeye, alafua akasema ngoja nikamuangalie, basi akaenda akamwambia bibi kuna watu hapo nje wanakuulizia bibi akasema kina nani, bibi na yeye akashtuka akasimama” amesema Asifiwe Kibiki mjuku wa marehemu.

“Ile anatoka bibi na mimi natoka naelekea jikoni, nipo jikoni kule naangalia maji kwa maana kuna kazi kidogo alinipanifanye, na mimi ninavyotoka yeye akaingia anaingia akamlawiti bibi  kisha akamzima hapa dada, yeye akadonga alivyokosa pumzi, kisha akafanya tendo alilokuwa anataka akenda kumtupia kule pembeni kwenye box, dhidi tuna vyozidi kupiga kelele tulivyosikia lile bomu watu wanavyokuja wanakimbia na wale walikimbia na kuna kijana alijaribu kuwafukuzia wakaokota jiwe wakamjeruhi hapa ubavuni, lakini tulijaribu kuwafukizia lakini tulishindwa mimi mwenyewe nilikuwa na mtoto” Asifiwe Kibiki

“Hao watu walikuwa watatu na  mmoja aliyefanya hicho kitendo alisimama hapa mlangoni ndio alikuwa wakwanza  yaani mfanya tukio hao wengine mmoja alikuwa tu pale varani  anakula round tu alikuwa  anakunywa soda alikuwa amenunua hiki kisoda kidogo cha miatano ili kuonekana tu ni wenyeji wanashida tu, shida tu alafu mmoja alikuwa amejibanza kule Kwenda kwenye geti lilekule mwishoni amesimama, yaani mimi ninavyotoka yule aliyekuwa anakunywa soda alikimbilia kwa mwenzake kule mwishoni” ameendelea kusema Asifiwe.
Mwenyekiti kitongoji cha Banawano Festo Mwangamila amesema alifika eneo la tukio baada ya kupigiwa simu na kukuta watuhumiwa wameshatoroka eneo hilo huku akibainisha kuwa tukio hilo ni la kwanza katia kitongoji chao.

Naye Diwani wa Viti maalumu tarafa ya Mlowe Laula Kilienyi, ameelezea namna avyomfahamu marehemu Christina Kibiki kuwa ni mtu aliyekuwa mchangamfu, mtendaji bora wakazi na mpenda watu hivyo watamkumbuka kwa mengi.

Kwa upande wake, Shakila Kiwanga, diwani wa kata ya Kalenga, amesema alipokea taarifa ya tukio hilo majira ya saa 5 usiku kutoka kwa mtoto wa marehemu juu ya kuvamiwa kwa mama yake, hivyo akaungana na vionhozi wengine hadi hospital ya Tosa maganga ili kujua hali ya mgonjwa, lakini nbaada ya muda mfupi walipewa taarifa za kifo cha katibu huyo.


Mkurugenzi wa tiba hospital ya rufaa ngazi ya mkoa tosa Maganga na Dkt bingwa wa upasuaji, Thomas Malongo amesema walimpokea Christina Kibiki akiwa hajitambui huku akiwa na majeraha sehemu mbali mbali za mwili wake Pamoja na kuvuja damu puani na masikioni.

Amesema timu ya madaktari katika hospital hiyo walijitahidi kuokoa Maisha yake kwa kuzuia damu kuendelea kuvuja lakini baada ya saa moja na nusu mauti mgonjwa huyo alipoteza Maisha.

Hata hivyo jeshi la polisi mkoa wa Iringa limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya katibu wa chama cha mapinduzi Christina Kibiki, ambaye amefariki baada ya shambuliwa na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi kifuani Pamoja na kitu Kizito kichwani.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi, amesema watuhumiwa hao baada ya kufanya tukio hilo walikimbia bila ya kuchukua kitu chochote nyumbani kwa marehemu.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimelaani tukio la Katibu wake, Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Christina Kibiki kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Makalla amesema marehemu alikuwa anajiandaa kuhudhuria semina elekezi kwa makatibu mjini Dodoma kesho Alhamisi, Novemba 14, 2024.



MATUKIO DAIMA MEDIA NI KATI YA VYOMBO VIWILI VYA MITANDAONI TANZANIA VILIVYO TEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS.

JINSI YA KUPIGA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA

Ingia katika tovuti ya www.samiaawards.tz 

1. Nenda sehemu iliyoandikwa “Piga Kura” 

2. Bonyeza neno lililoandikwa NEXT 

3. Utaona Makundi ya tuzo, bofya lililoandikwa TUZO KWA VYOMBO VYA HABARI kisha libonyeze hapo

4. Utaona sehemu imeandikwa "VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI" kisha ingia hapo

5. Baada ya hapo utaona jina MATUKIO DAIMA Namba ya Mshiriki NNI 24005006  Kisha bonyeza kitufe kilichoandikwa PIGA KURA

Ukikamilisha hatua hiyo, utakuwa umepigia chagua *MATUKIO DAIMA*

Asante sana kwa kura yako

KUPIGA KURA KWA SIMU YA KAWAIDA 

1:Ingia Uwanja wa Ujumbe 

2:andika neno Kura  Kisha acha nafasi weka namba 24005006

3:Tuma kwa Namba 15200

HAKIKA UNA SALIO LA KAWAIDA SHILINGI 100 TU SIO KIFURUSHI 

HAPO UTAKUWA UMEPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA 

🙏 AHSANTE SANA KWA KURA YAKO MAANA KURA YAKO NI USHINDI WETU MATUKIO DAIMA MEDIA NI YETU SOTE MUNGU MWEMA AKUBARIKI KWA KURA YAKO YA THAMANI


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI