Header Ads Widget

RAIS SAMIA ATOA MILIONI 50 KUCHANGIA UJENZI WA KANISA KIGOMA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi milioni 50 kuchangia ujenzi wa kanisa Katoliki Parokia ya  Maria Mtakatifu Mama  wa Mungu  ,Kibwigwa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma ambapo kiasi cha shilingi milioni 250.2 kilichangwa katika harambee hiyo.

Akitangaza matokeo ya harambee hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC),Masanja Kadogoda aliyekuwa mgeni rasmi ambaye alichangia kiasi cha shilingi milioni 20 alisema kuwa Raisi Samia kwa mapenzi mema amechangia ujenzi huo baada ya kuombwa kufanya hivyo na skofu wa jimbo la Kigoma Mhashamu Askofu Mlola.

Kadogosa alisema kuwa katika harambee hiyo Raisi Samia pia aliungwa mkono na Mwenyekiti wa Makampuni ya GSM, Gharib Mohamed huku wapenzi wa timu za simba na Yanga waumini wa kanisa hilo wakichangia kiasi cha shilingi Shilingi 890,000 ambapo wapenzi wa Yanga walichangia shilingi 528,000 na wapenzi wa Simba shilingi 362,000.


Awali Askofu wa jimbo Katoliki la Kigoma,Mhashamu Joseph Mlola amemshukuru Rais Samia kwa mchango huo akionyesha kuwa kiongozi anayejali watu kwa hali yeyote sambamba na kuwashukuru watu wote waliofaanikisha harambee hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC. Masanja Kadogosa.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa kanisa hilo Katibu wa Kamati ya ujenzi, Joseph Kahene alisema kuwa kanisa  hilo lilianzishwa 1933  ambapo hata hivyo hakukuwa na idadi kubwa ya waumini kama sasa ambapo kwa sasa kanisa hilo lina waumini 14,000 hivyo kufanya kanisa linalotumika sasa kuwa dogo na lililozeeka hivyo kunahitajika ujenzi wa kanisa jipya. 

Kahene alisema kuwa malengo ya Mradi huo wa kanisa jipya unahitajika kiasi cha shilingi Bilioni 4 ili kuwezesha kanisa kukamilika likiwa na uwezo wa kuchukua waumini 1800 kwa wakati mmoja hivyo michango kutoka kwa watu mbalimbali inahitajika kufanikisha mradi huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI