Na Hamida Ramadhani Matukio Daima APP Dodoma
MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema kwa kushirikiana na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanatekeleza miradi mitatu katika eneo la Msomera ambapo Kwa sasa eneo hilo huduma ya mawasiliano inapatikana kwa uhakika kwa mitandao yote .
Wananchi wa Msomera walihamishwa kutoka Wilaya ya Ngorongoro na kupelekwa Handeni mkoani Tanga ambapo Katika eneo hilo hapakuwa na huduma ya mawasiliano .
Mashiba amaeyasema hayo wakati akielezea utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya UCSAF na kazi ambayo wameifanya ya kuboresha mawasiliano pamoja na kupeleka vifaa vya TEHAMA katika kijiji cha Msomera Mkoani Tanga.
Amesema jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa Huduma ya Mawasiliano Vijijini unaendelea ambapo Mfuko huo umesaini mkataba wa kupeleka huduma za Mawasiliano katika kata zaidi ya 1900 na mradi huo umefikia asilimia 90 katika utekelezaji wake.
Ameeleza kuwa jukumu walilokasimiwa na serikali la kuhakikisha wanapeleka mawasiliano vijijini wanalitekeleleza vyema ambapo mpaka sasa kazi kubwa imefanyika ya ujenzi wa minara vijijini na lengo likiwa ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata huduma ya mawasiliano ili kuchochea maendeleo kupitia uchumi wa kidijitali.
"tutakapo kamilisha ujenzi wa miradi hiyo ya mawasiliano wananchi wapatao milioni 15 watapata huduma za mawasiliano na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote na serikali ya Awamu ya sita Chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan na watoa huduma wengine wa mawasiliano nchini kwa namna wanavyopambana kuhakikisha huduma hizo zinawafikia Watanzania wote,”amesema Mashiba
Na kuongeza "Pia kuna wanachi wengine kutoka Ngorongoro wanatarajiwa kuhamia Msomera na Ujenzi wa nyumba takribani 5000 unaendelea huko ila ni katika kijiji cha Mkababu na huko hapakuwa na Watanzania wanaoishi hivyo huduma ya mawasiliano hazipatikani kwa hivyo kwa kushirikiana na TTCL tunajenga Mnara wa Mawasiliano huko ambako mpaka ninavyozungumza ujenzi wa mnara huo unaendelea ili wananchi wale watakapo hamia wasipate shida ya mawasiliano” ameeleza Mashiba
Aidha aliwashukuru watoa huduma za mawasiliano kwa kushirikiana vizuri kwani mashirikiano hayo ni moja ya mahusiano mazuri Kati ya Serikali na Sekta binafsi nani mfano mzuri nakutaka Kuendelea hivyo ili adhima ya Tanzania yote ya kupata mawasiliano iweze kutimia.
0 Comments