NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Wasiwasi umeingia katika vijiji mbalimbali kuwa huenda bei za Ulanzi zikapanga kufuatia Wahadhili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kugundua faida na fursa kubwa zinazotokana na kinywaji hicho.
Wenyeji wa mikoa inayolima Ulanzi ikiwemo Iringa, Njombe na Mbeya wamekiri kuwa sasa bei ya Ulanzi badala ya kuuzwa elfu 2 kwa lita sasa utauzwa elfu 5 suala ambalo litawapa ugumu.
Wananchi wanywaji wa Ulanzi wamesema kwa sasa kuna haja kubwa ya kuachana na kunywa Ulanzi kutokana na bei yake kupanda mara tatu ya bei ya kawaida waliyokuwa wamezoea.
Aidha, wanywaji hao wameitaka Serikali kuingilia kati upandishwaji holela wa bei z ulanzi kwa lita, kwa kuwa wateja hao wamekuwa wadau wa kinywaji hicho kwa muda mrefu ambapo wanadai kuomba kuheshimiwa ili waendelee kunywa.
0 Comments