Mheshimiwa Ngollo Malenya, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, akizungumza katika kongamano la kibiashara la Namtumbo Kihenge likiwa na nia ya kuvutia uwekezaji zaidi wilayani hapo.
Majani Moremi Wambura, Meneja
uendellevu mradi wa Mantra, akizungumza pindi akifanya wasilisho katika
kongamano la Namtumbo Kihenge lililofanyika September 21 na 22, 2023.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Amon Mtega, MATUKIO DAIMA MEDIA Namtumbo.
KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya
urani imeahidi kusaidia maendeleo ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kupitia
sera yake ya uwajibikaji wa jamii (CSR).
Ahadi ya Mantra Tanzania imetolewa
katika kongamano la biashara la Namtumbo Kihenge lililofanyika Septemba 21 hadi 22, mwaka huu.
Katika kongamano hilo, mgeni rasmi
ambaye pia ni Mkuu Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngolo Ng’waniduhu, alisema tukio
hilo limeleta matumaini na ni muhimu kwa wilaya hiyo kwani limetoa fursa ya
majadiliano, makubaliano na kubadilishana mawazo ya kibunifu ambayo yanaweza
kusukuma mbele gurudumu la maendeleo endelevu katika eneo hilo.
Mantra, kama mdau muhimu wilayani
humo, ilishiriki katika kongamano hilo na kuweka bayana namna jamii inaweza
kunufaika kupitia mradi wake.
Akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa
Wilaya ya Namtumbo kwa kuandaa jukwaa la Namtumbo Kihenge 2023, meneja wa
uendelevu wa Mantra Tanzania Majani Moremi Wambura alieleza faida za mradi huo
zikiwemo ajira na fursa za biashara kama sehemu ya matokeo ya maendeleo
yatokanayo na shughuli za uchimbaji.
“Mradi wa Mantra si uchimbaji wa urani
pekee,” Majani aliwaelezea washiriki.
“Bali ni utengenezaji wa fursa zitakazoweza kuinufaisha jamii yote.
Kutoka ajira za moja kwa moja kwenye mradi hadi ajira zisizo za moja kwa moja
zinazozalishwa na mahitaji ya bidhaa na huduma. Mradi huu ni kichocheo cha
ukuaji wa kiuchumi.”
Katika manufaa ya kiuchumi, Majani
aliwaeleza washiriki kuhusu mkakati wa uwajibikaji wa kampuni ya Mantra kwa
jamii wa miaka mitano (2023-2028) ambao umejikita katika maneno ya afya, elimu,
uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya jamii.
“Mkakati wetu wa uwajibikaji kwa jamii
si tu kurudisha kwa jamii,” alisema Majani na kuongeza: “Ni uwezeshaji kwa
jamii iliweze kuchukua hatamu ya maendeleo yake. Tunataka kutengeneza mfumo
endelevu wa maendeleo ambao utaendelea kuinufaisha jamii hata baada ya mradi
huu kuisha.”
Uwajibikaji wa Mantra kwa jamii
umeenda zaidi ya yaliyoainishwa katika mpango wake wa CSR. Kampuni ya Mantra
Tanzania ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa jukwaa la Namtumbo Kihenge la mwaka
huu na imeahidi kuendelea kusaidia majukwaa kama hayo pamoja na programu ambazo
zitakuwa na matokeo chanya ya kiuchumi katika ngazi ya wilaya, mkoa pamoja na
nchi.
“Tunaamini katika nguvu ya ushirikiano
na ushirikishwaji wa jamii,” alisema Majani. “Kwa kudhamini majukwaa kama hili
la Namtumbo Kihenge, tunahimiza utamaduni wa majadiliano na ubunifu ambao
utaharakisha maendeleo ya wilaya.”
Huku Mantra Tanzania Limited ikiendeleza
mradi wake wa urani, kampuni hiyo bado imeendelea kutekeleza ahadi zake za
kuisaidia wilaya ya Namtumbo kupitia sera yake ya uwajibikaji (CSR) na kusaidia
shuguli za kijamii.
Kupitia jukwaa hilo, Mantra Tanzania
ilipata tuzo ya shukrani kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ambayo
ilitambua mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika tukio hilo.
Kampuni hiyo ina rekodi ya muda mrefu
ya kushiriki katika jamii na mchango wake katika shughuli za kijamii hivyo huu
ni muendelezo wa jitihada zake za kuinua uchumi wa wilaya na mkoa kwa ujumla.
Kutambuliwa kwake katika tukio hilo ni ushahidi wa wazi wa namna inavyojitoa
pamoja na juhudi katika kazi.
Akizungumza katika jukwaa la Kihenge,
Mbunge wa jimbo la Namtumbo, Vita Kawawa aliwataka wananchi kutumia kongamano
hilo la kibiashara kuvutia wawekezaji wakubwa katika sekta za kilimo na madini
kwani wilaya hiyo ina fursa kubwa ya kuchangia uchumi wa nchi kwa kiasi
kikubwa.
Mbunge huyo aliomba mamlaka za
serikali kuunga mkono mradi wa uchimbaji urani wa Mantra Tanzania.
Mheshimiwa Vita anaamini kuwa endapo
Serikali itaongeza jitihada, mradi huo unaweza kufanya kazi kwa kipindi
kisichopungua miaka 15 na kuchangia hadi asilimia 20 ya uzalishaji wa urani
barani Afrika, sawa na asilimia 4 ya uzalishaji wa madini hayo kidunia.
Baada ya kongamano hilo, Mantra
iliandaa ziara ya madini kwa washiriki 150 kutoka jukwaa la biashara la
Namtumbo, shughuli ambayo iliongozwa na Mkuu wa wilaya Mhe. Ngolo Ng’waniduhu.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la
kuwaelimisha wananchi juu ya shughuli za mgodi wa urani, usalama unaochukuliwa
na Mantra wakati wa uchimbaji.
Zoezi hili lilifanyika katika eneo la mgodi
wa urani unaoendeshwa na Mantra lililopo ndani ya Mbuga ya Nyerere, takribani
kilomita 54 kutoka makazi ya watu na kilomita 140 kutoka Namtumbo mjini.
0 Comments