Header Ads Widget

WATAKAOLIPWA FIDIA ZA MAENEO YA MADINI LUDEWA NJOMBE WATAHADHARISHWA NA MATAPELI

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati serikali ikitarajia kuwalipa fidia wananchi wanaopisha machimbo ya makaa ya mawe na Chuma cha Liganga kiasi cha shilingi bilioni 15.4 Wilayani Ludewa mkoani Njombe,Wananchi wa maeneo hayo wametahadharishwa dhidi ya matepeli na uangalifu wa fedha hizo pindi zitakapowafikia.



Kwa kuliona hilo serikali ya mkoa wa Njombe na wilaya ya Ludewa imefika katika kata ya Nkomang'ombe kutoa elimu juu ya fedha hizo ambapo mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka anasema ni lazima wananchi wajiandae kuzipangia matumizi na kubumi miradi endelevu pindi watakapolipwa fedha hizo huku wakitakiwa kuwa waangalifu na matapeli.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Mhe.Deo Sanga ambaye ni mbunge wa Jimbo la Makambako yeye anawataka wananchi watakaolipwa fidia kuepukana na anasa za dunia.



Awali mkuu wa wilaya ya Ludewa Mhe.Victoria Mwanziva amesema kitendo cha serikali kuwalipa fidia wananchi hao katika siku za usoni ni kiashiria cha Kuanza utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa ya Makaa ya Mawe na Chuma.



Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Mhe.Joseph Kamonga anasema wananchi wanaopaswa kupisha maeneo hayo baada ya kulipwa fidia wanayo haki ya kunufaika na miradi hiyo kwa kufanya uwekezaji katika maeneo hayo.



Wananchi wa wilaya ya Ludewa hasa kwenye maeneo ya madini hayo akiwemo Daniel Haule na Selina Mhagama wanaishukuru serikali kwa hatua ilizozichukua licha ya wengine kutoamini kama fedha za fidia zitawafikia hadi pale watakapozishika mkononi.



Ziara ya mkuu wa Mkoa  na kamati ya siasa mei 17,2023  imezulu katika eneo la makaa ya mawe Mchuchuma na Mei 18 mwaka huu inatarajia kutembelea na kuzungumza na wakazi wa eneo mundindi kwenye  madini ya chuma Liganga wilayani Ludewa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI