KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdala Shaibu Kaim amewataka Watanzania kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ambayo kwa asilimia 95 yanatokana na uharibifu wa mazngira.
Aidha aliwataka wananchi kuwa na utamaduni wa kula kwa mpangilio na kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wananchi wa Halmashauri ya Mji Kibaha wakati wa kupokea Mwenge wa uhuru ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Kaim alisema kuwa uharibifu huo wa mazingira unasababisha kushusha uchumi wa nchi kutokana na athari hizo hivyo kuna haja ya Watanzania kusimamia mazingira ili yasiharibiwe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Simon John alisema kuwa Mwenge huo wa uhuru ulitembelea jumla ya miradi 12 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9.
John alisema kuwa fedha za miradi kati ya hizo milioni 520.2 ni mchango kutoka Halmashauri na milioni 683.7 ni kutoka serikali kuu na bilioni 2.4 ni michango ya wananchi.
Alisema kuwa fedha nyingine ni kutoka kwa wahisani ambapo ni kiasi cha shilingi milioni 293.3 na michango ya mwenge iliyoelekezwa katika miradi ya maendeleo ni shilingi milioni 2.5.
Mwisho
0 Comments