Header Ads Widget

TPDC YAFANYA BONANZA LINDI KUKUZA USHIRIKIANO NA UJIRANI MWEMA



NA HADIJA OMARY LINDI.


KATIKA kuendeleza mkakati wa shirika la maendeleo ya petrol Tanzania (TPDC)  wa kuwa karibu na wadau wamefanya  bonanza la michezo  kwa wakazi wa  kata   mnazi mmoja Manispaa ya Lindi Mkoani humo. 


Akizungumza na wakati wa Bonanza hilo lililoenda sambamba na upimaji wa Afya  Mkuu wa kitengo cha uhusiano na mawasiliano TPDC  Maria Mselemu amesema bonanza hilo limehusisha michezo tofauti tofauti ikiwemo    mpira wa miguu, kufukuza kuku na kukimbia na magunia  huku washindi wa michezo hiyo wakijivunia zawadi lukuki .



Mselemu pia alieleza kuwa  lengo la bonanza hilo ni Kukuza ushirikiano na ujirani mwema katika maeneo ambayo yamepitiwa na bomba la gesi asilia  sambamba na kutoa elimu kwa wananchi wanaopitiwa na mradi huo.



" tangu mwaka 2014/2015 TPDC imekuwa na zoezi la usafirishaji wa gesi asilia kutoka mtwara mpaka Dar es salaam  lakini njiani humu kwenye mikoa hiyo na mikoa mingine tunakutana na wananchi kama hawa tunashukuru kwamba wamekuwa walinzi wazuri kukiwa na tatizo ama viashiria vyovyote vinavyotoa taswila ambayo sio chanya wananchi hawa wanatupa taarifa hivyo hawa ni walinzi wetu" alisema Mselemu. 



Nae Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amesema Bonanza hilo licha  ya kuimarisha  afya lakini pia litasaidia kujenga uwelewa  kwa wananchi wanaopitiwa na mradi huo juu ya shighuli mbali mbali zinazotekelezwa na TPDC.


 Alisema shirika la maendeleo ya petrol na mafuta Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali katika wilaya ya Lindi yenye faida kwa wananchi na serikali.


" hapa mnazi mmoja upo mradi mkubwa  unaoendelea wa kusambaza gesi asilia  majumbani. mradi umeanza, unagramana kubwa na wananchi wanaona tu mabomba yanapita ya gesi wapo waliojitokeza kujiandikisha wanataka waunganishiwe gesi hiyo" .



Lakini kama Serikali tumeona upo umuhimu wa kuwepo na ushiriki wa wananchi wenyewe katika utekelezaji wa miradi hiyo.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mnazi mmoja Saidi Mchinjita  amesema hatua ya TPDC kufanya bonanza hilo inaendelea kuwafanya wananchi wa maeneo hayo kuendelea kuwa walinzi wa mradi pamoja na kuufahamu kwa ufasaa mradi husika.


" sisi wakazi wa mnazi mmoja tumejiandaa vizuri kupokea miradi yote inayotekelezwa na TPDC na tutaendelea kuilinda na kuitunza miundo mbinu hii kwa sababu tunaihitaji " alisema Mchinjita


Mwisho 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI