Header Ads Widget

KIGOMA YAFANYA VIZURI UKUSANYAJI MAPATO YA MADINI.

 




Na Fadhili Abdallah,Kigoma



MKOA wa Kigoma unaelezwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya madini kutoka kwa wachimbaji wadogo ikielezwa kuwa marekebisho ya sheria na mazingira wezeshi yamechangia katika hilo.

 


Katibu Mtendaji wa Tume ya madini nchini , Mhandisi Yahaya Semamba alisema hayo akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wachimbaji wadogo wa madini na kusema kuwa serikali imeweka mazingira wezeshi ambayo yanawafanya wachimbaji hao kufanya shughuli zao kwa tija.



Katibu huyo Mtendaji wa Tume ya Madini nchini alisema kuwa kumarishwa kwa shughuli za utendaji kwa wachimbaji wadogo kumewezesha wachimbaji hao kuongeza makusanyo ya pato la serikali katika sekta ya madini kufikia asilimia 40 na mpango wa serikali ni kuwezesha wachimbaji wadogo kuingiza asilimia 50 ya pato la Taifa.




Alisema kuwa mkoa Kigoma umeweza kufanya vizuri katika sekta ya madini kwa mwaka huu wa fedha unamaolizika mwezi Juni kwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 katika lengo la kukusanya shilingi Bilioni 1.6 ambapo lengo la serikali ni kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 822 kwa mwaka huu wa fedha kwa sekta nzima ya madini.

 

Katika hatua nyingine katibu huyo wa Tume ya madini amewataka wachimbaji wadogo  wa madini mkoani Kigoma  kuunda umoja na ushirikiano na wachimbaji na wanunuzi wa madini kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu ili kuimarisha soko la madini nchini.

 


Semamba alisema kuwa mwaka 2017 serikali iliifanyia marekebisho  ya sheria ya madini sambamba na kuondoa tozo na kodi mbalimbali ambazo zilikuwa zinalalamikiwa lengo likiwa kuweka mazingira wezeshi kwa watu wa nje kufanya shughuli za madini lakini kutumia masoko yaliyopo nchini Tanzania kwa ajili ya kuuza madini yao.

 



Awali akizungumza kabla kufunguliwa kwa mafunzo hayo Katibu Msaidizi wa Chama cha wachimba madini mkoani Kigoma (KIGOREMA), Boaz Mkohozi alisema kuwa wanashukuru serikali imeanza kurekebisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya madini ili kuwezesha wachimbaji na watu wanaoshughulika na madini kazi zao kuwa na tija.

 


Hata hivyo alisema kuwa bado wachimbaji wadogo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya matumizi ya vifaa duni katika kazi zao sambamba na changamoto ya upatikanaji wa mikopo kutoka taasisi za fedh ili wanunue zana bora na za kisasa.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI