Header Ads Widget

KESI YA WANAVIJIJI WA LOLIONDO DHIDI YA WAZIRI WA UTALII MA MALIASILI KUWASILISHWA KWA NJIA YA MAANDISHI NDANI YA SIKU 21

 



NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Kesi namba 21 ya mwaka 2022 ya maombi ya mapitio ya Sheria dhidi ya Tangazo la Waziri wa Mali asili na Utalii ya tarehe 17 Juni 2022 kuhusu ardhi ya Vijiji vya Loliondo kuwa Pori Tengefu la Pololeti, hoja kuwasilishwa kwa njia ya maandishi ndani ya siku 21 huku waleta majibu wakitakiwa kujibu ndani ya wiki mbili.


Kesi hiyo ambayo ilikuwa katika hatua ya kusikilizwa mbele Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Arusha Joachim Tiganga  huku upande wa waleta maombi wakiwakilishwa na mawakili Mpale Mpoki, Jeremia Mtobesia , Jonas Masiaya na Denis Mosses  na upande wa wajibu maombi iliwakilishwa na mawakili Jackline Kinyasi na Peter Museti.



Akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakana wakili upandea wa waleta maombi Denis Mosses alisema kuwa walikuja kwaajili ya kusikilizwa lakini walikuwa nje ya muda kwani muda ulitakiwa kuwa saa sita lakini kutokana na sababu mbalimbali ilitwa saa tisa na kwa muda huo wasingeweza kusikiliza kwakuwa kesi hiyo Ina mambo mengi.


“Imeonekana ni busara kufanyika kwa njia yaaandishi ambapo badala ya kuongea kwa mdomo hoja zote ziletwe kwa maandishi na kwamaana hiyo upande wa waleta maombi wametakiwa kuleta hoja zao ndani ya wiki tatu(21) na upande wa pili watajibu kwa wiki mbili na majibu ya Mahakama yatakuja baada ya wiki na itakuja Julai 31,2023 kama kutakuwa na masuala yanayohitaji ufafanuzi kwa mahakama na baada ya hapo itapanga siku ya kutoa hukumu,” Alisema wakili Denis Mosses.


 

Aidha katika shauri hilo Waleta maombi wanaiomba Mahakama iagize Serikali kuondoa zuio dhidi ya  Wananchi  kuingia kwenye eneo la Km2 1502 ambalo wamekuwa wakitumia kwa ajii ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya kufanyia shughuli za imani yao 


Pia waleta maombi wanaiomba Mahakama itengue Tangazo la Serikali  (GN421) la tarehe 17 Juni 2022  kuwa ni batili na limetangazwa kinyume na sheria na pia haikuwashirikisha wananchi kama sheria inavyotakaikiwa ni pamoja na Mahakama itamke kuzuia Serikali na Mawakala wake wasifanye oparesheni zozote kwenye eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI