Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Upendo,Amani na kutolipizana visasi baina ya wafanyabiashara wilayani Njombe vimetakiwa kutamalaki ili kupanua wigo katika kukuza uchumi wa wananchi kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa Uwt wilaya ya Njombe Beatrice Malekela wakati wakikabidhi maduka tisa kwa wafanyabiashara yaliyoungua Moto Hapo April mosi mwaka huu na kukarabatiwa upya na jumuiya hiyo.
Bi.Malekela amesema kwa umoja wao wafanyabiashara wote wa mji wa Njombe waliwachangia waliounguliwa maduka kiasi Cha zaidi ya Shilingi milioni 3 ambapo jumla ya shilingi milioni 18.6 zimetumika katika ukarabati wa maduka hayo.
Agizo la Katibu wa UWT wilaya ya Njombe Bi.Sauda Suleiman Anawataka wafanyabiashara hao kulipa kodi ya pango kwa wakati kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.
Kwa Upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Bwana Sure Mwasanguti amesema wakati janga la Moto likiendelea majira ya usiku Wapo waliofurahia kitendo hicho jambo linalopaswa kupingwa na kila mwenye mapenzi mema.
Baadhi ya wafanyabiashara waliounguliwa maduka hayo akiwemo Amos Chaula na Elizabeth Mpogolo wamekiri kupitia katika kipindi kigumu Lakini wanashukuru kwa kushikwa mkono na wafanyabiashara na wadau wengine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara JWT Halmashauri ya mji wa Njombe Bwana Eliud Pangamawe ametumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara kuwa watulivu pindi wanapokumbwa na majanga huku akitaka taasisi za bima kuwafikia na kuwapa elimu ya bima.
Majira ya usiku wa April mosi mwaka huu uliibuka moto katika maduka hayo yanayomilikiwa na UWT Wilaya ya Njombe huku jeshi la Polisi mkoa wa Njombe baadaye likatoa ripoti kuwa mtu mmoja mfanyabiashara kwenye moja ya duka lililoungua linamshikilia kwa kusababisha moto huo kwa kile alichodai kutaka kulipwa fidia ya bima ya biashara yake.
0 Comments