Serikali ya Kenya imethibitisha kuachiwa kwa mwanaharakati wa nchi hiyo Boniface Mwangi ambaye awali alikuwa anashilikiwa nchini Tanzania baada ya kuingia nchini humo kwa lengo la kutaka kuhudhuria kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Kwa mujibu wa ofisi ya Mambo ya Nje ya Kenya na vyombo vya habari vya Kenya, Boniface alisafirishwa kwa njia ya barabara na kupatikana katika mji wa Ukunda uliopo Pwani ya Kenya, takriban kilomita 30 kutoka mji wa MombasaMwangi ambaye alitoweka tangu Jumatatu baada ya kuja Tanzania amekimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu, kulingana na wakili wake, James Wanjeri, ambaye anadai kuwa amejeruhiwa vibaya na hataweza kutembea.
0 Comments