Header Ads Widget

ATAKA KUJIUA KWA KUJIKATA NYETI ZAKE

 



Mwanaume mmoja ajulikanae Kwa jina la Ansele Sebuka mwenye umri wa miaka (42) Mkazi wa Namagondo Wilaya ya ukerewe Mkoani Mwanza amekutwa ndani ya chumba chake akiwa amejikata nyeti zake Kwa kutumia kisu.


Jeshi la polisi Mkoani hapa likitoa taarifa ya Chanzo cha tukio hilo limesema kuwa mhanga alikuwa na ugomvi na familia yake uliopelekea kupata msongo wa mawazo na kutaka kujiua Kwa kujikata na kisu.


 Ansele Sebuka  anadaiwa alikuwa anatuhumiwa na ndugu zake Kwa kuiba mali mbalimbali za familia na za jamii inayomzunguka na kwenda kuziuza pamoja na ulevi uliokithiri ambapo waliamua kumtenga kutokana na tabia zake.


Baada ya tuhuma hizo ndipo aliamua kujikata uume wake kwa kutumia kisu chenye ncha kali na kuacha ukining’inia kwa lengo la kujiua. 



Ansele Sebuka alipelekwa katika Hospitali ya wilaya hiyo na kupata matibabu, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kufuata njia sahihi za kutatua matatizo yao hususani Kwa kuwaona wataalamu wa afya ya akili ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na msongo wa mawazo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI