Header Ads Widget

KESI YA WANANCHI WAWILI WANAOPINGA KUTOZWA FAINI KUSIKILIZWA MEI 10, MWAKA HUU

 


Teddy Kilanga _Arusha.


Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imepanga Mei 10,2023 kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na wakazi wawili wa wilaya ya Ngorongoro wanaopinga utozaji wa Sh15 Milioni kama faini baada ya kuingiza mifugo katika Pori Tengefu la Pololeti.


Waomba rufaa katika rufaa hiyo ya jinai namba 9/2023 ni Baraka Kesoi anayedai kutozwa Sh13 Milioni na Baraka Oloishiro aliyedai kutozwa Sh milioni mbili baada ya kudaiwa kuingiza ng'ombe,mbuzi na kondoo kwenye pori hilo tengefu,ambapo wamedai kutozwa faini Sh 100,000 kwa ng'ombe mmoja na sh 25,000 kwa mbuzi na kondoo mmoja.


Kesoi na Oloishiro wamewakilishwa na mawakili Joseph Ole Shangai na Dennis Mosses huku wajibu rufaa ambao ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA),Mkurugenzi wa wanyamapori na Jamhuri,wakiwakilishwa na Wakili wa serikali Tonny Kilomo.



Leo Jumatano Aprili 5,2023 mbele ya Jaji Mohamed Gwae wa mahakama hiyo,shauri hilo lililotajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo lilipangwa kwa ajili ya kutajwa ambapo alisema litasikilizwa Mei 10,2023.


Wakili Mosses ametaja miongoni mwa hoja za rufaa hiyo ni pamoja na waomba rufaa hao kudai NCAA haina mamlaka kutoza faini kwenye sehemu ambazo ni za nje ya eneo hilo ikiwemo eneo hill la Pori tengefu ambalo limeanzishwa na Sheria ya Wanyamapori na kuwa mwenye mamlaka ni Mkurugenzi wa wanyamapori.


Nyingine ni utozaji wa faini ya Sh 100,000 kwa ng'ombe mmoja ni batili na kinyume na sheria,kutoza faini Sh 25,000 kwa kondoo au mbuzi mmoja ni batili na kinyume cha sheria pamoja na faini ya Sh 13,000,000  ni kinyume cha kiwango kilichowekwa kisheria.


Wakili huyo alidai Januari 25,mwaka huu waomba rufaa walikamatwa katika pori hilo wakilisha mifugo yao na kutozwa faini hiyo ambapo alidai wana ushahidi wa namba mahususi ya kuweka malipo ya serikali 'control number' waliyodai kupewa na na NCAA pamoja na risiti ya malipo.



"Wanaomba mahakama iseme uamuzi wa NCAA wa kutoza faini ni kinyume cha sheria na faini hiyo ni kiwango cha juu kabisa ambacho kimezidi kilichowekwa na sheria,"amesema

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI