Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Changamoto za kibajeti na vitendea kazi kwa maofisa ardhi kwenye halmashauri mbalimbali nchini zimetajwa kukwamisha michakato ya uwekezaji kwa wawekezaji mbalimbali jambo ambalo kituo cha uwekezaji nchini TIC Kinapaswa kuingilia kati.
Katika semina elekeza kwa maofisa ardhi mkoani Njombe chini ya Kituo cha uwekezaji kanda ya nyanda za juu kusini imebainika kuwapo kwa vikwazo hususani ukata wa kifedha kwa ajili ya kuyafikia maeneo ya uwekezaji jambo ambalo baadhi ya maofisa hao akiwemo Cosmas Buja,Edward Mwaigombe,Happy Mkalawa na Ayub Unduru wanaweka bayana changamoto hizo mbele ya kituo cha uwekezaji wakihitaji msaada zaidi.
Lengo la semina hiyo kwa maofisa ardhi mkoani Njombe ni kutaka waende kufanya vyema katika matumizi bora ya ardhi kwa wawekezaji na kuondosha vikwazo vinavyokwamisha sekta ya uwekezaji ambapo Kaimu Meneja wa kituo cha uwekezaji nchini kanda ya nyanda za juu kusini Ajelandro Sindano anakiri kuwa changamoto hizo zimeanza kutatuliwa.
Kaimu Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Njombe Geofrey Masunda anakiri kuwapo kwa maeneo mengi ya uwekezaji katika halmashauri za mkoa wa Njombe na hivyo kuondoshwa kwa vikwazo hivyo kutarahisisha michakato ya uwekezaji kwenda haraka.
Uwekezaji huwekezwa ardhini ambapo Afisa ardhi kituo cha Uwekezaji nchini TIC Jonas Chikawe anasema kufunguliwa kwa ofisi za kamishna wa ardhi kila mkoa kumesaidia sana kuongeza kasi ya shughuli za uwekezaji nchini.
Kwa upande wake Kaimu Katibu tawala mkoa wa Njombe akiwa mgeni wa heshima katika semina hiyo bwana Joseph Mutashubilwa anatumia fursa hiyo kuwaonya maofisa ardhi warasimu katika michakato mbalimbali ukiwemo uwekezaji kwa wawekezaji.
Serikali ya awamu ya sita imefungua mipaka ya kidiplomasia na kuruhusu wageni kuingia kuwekeza nchini kwa kupunguza vikwazo ambavyo vimekuwa mwiba kwa wageni jambo ambalo limesaidia kuongeza idadi ya wawekezaji wa nyanja tofauti.
0 Comments