Header Ads Widget

WCF WAWEKA REKODI YA MAFANIKIO MIAKA 10

 

  

NA ARODIA PETER, MATUKIO APP  Dar

Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) umefanikiwa kuwalipa fidia wafanyakazi na wategemezi wao wapatao 19,650 waliopata ajali, kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya.

Fidia hizo ni moja ya hitaji la msingi la uanzishwaji wa mfuko huo na linaonyesha utendaji wa moja kwa moja wenye tija kwa jamii ya wafanyakazi.

Hayo yamesemwa leo Mei 15, 2025 na Mkurugenzi mkuu wa WCF, Dkt John Mduma wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam akieleza mafanikio ya miaka 10 ya mfuko huo tangu kuanzishwa kwake pamoja na mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dkt Mduma amesema WCF ilianzishwa kutokana na changamoto za mfumo wa fidia uliopitwa na wakati kwa kutumia sheria ya 1949 ambao kwa ujumla haukidhi mahitaji ya sasa ya kijamii na kiuchumi.

“Kupitia WCF Serikali imejenga mfumo madhubuti wa kitaasisi unaolenga kutoa huduma za fidia kwa wakati, kwa uwazi na kwa kuzingatia haki za wafanyakazi.

“Pia idadi ya mafao imeongezeka hadi kufikia saba ambayo ni pamoja matibabu, ulemavu wa mda mfupi, ulemavu wa kudumu na fao la pensheni kwa wategemezi.

“Mafao mengine ni wasaidizi wa mgonjwa, utengamano na fao la msaada wa mazishi”amesema mkurugenzi huyo.

Aidha mkurugenzi huyo amesema mafanikio mengine ni uboreshaji wa mifumo ya Tehama, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya huduma zote kwa sasa zinapatikana kwa njia ya mtandao hivyo kupunguza urasimu, kuongeza uwazi na kuboresha ufanisi wa utendaji kazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI