Na MatukioDaimaApp
Wakulima wa zao la mpunga nchini wametakiwa kufika katika maonyesho ya sabasaba ili kupata elimu na mbegu bora zilizofanyiwa Utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari Kituo cha Dakawa Mkoani Morogoro.
Akizungumza na matukio daima mtafiti uharishaji na usambazaji teknolojia Ngabo Pamba kutoka Tari Dakawa alisema kuwa uwepo wao katika maonyesho ni fursa kwa wakulima wa zao la mpunga.
Alisema kuwa taasisi hiyo imeleta teknolojia mbalimbali za mpunga ambao umegawanyika katika makundi unaolimwa mabondeni na umwagiliaji na milimani.
“Kwa mbegu za Mabondeni na umwagiliaji zipo nyingi lakini mbegu ya salu 5 ni nzuri inanukia na uwezo wa kutoa tani 8 hadi nane na nusu kwa hekta moja ambapo kwa heka moja mkulima anaweza kupata magunia 30 aina
hii ni madhubuti kwao”
“Ipo pia tari rice one hii mbegu ni supa ina harufu nzuri inakoboreka vizuri inatoa mchele angavu na pia mavuno yake ni mengi ambapo unaweza kupata magunia 20 hadi 25”
“Ipo tari rice mbili hii inakomaa ndani ya siku 100 hadi 110 mabondeni na umwagiliaji inatoa tani 7-9 anauwezo wa kuzalisha hata kama mvua itakuwa ndogo.
“Tunawakaribisha watanzania wafike kwenye maonyesho haya na ili kuweza kulima ama kuongeza thamani kwa bidhaa za mchele ambapo unapata tambi, mche dona, pepeta unga hizi ndio teknolojia ambazo tunaita watanzania waje kupata elimu na wazitumie” alisema Pamba
0 Comments