Header Ads Widget

WAKULIMA ZAO LA KARANGA MPWAPWA WADAI MBEGU BORA ZIMEHAMASISHA KILIMO

 


Na MatukioDaimaApp, Dodoma

Wakulima wa zao la karanga Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamesema kuwa uwepo wa mbegu bora katika kijiji chao umehamasisha wakulima wengi kurudi kulima zao hili ambalo wengi walianza kulitekeleza kutokana na magonjwa na uzaaji hafifu wa mbegu za kienyeji. 


Akizungumza na mwandishi wetu Majuano Maluli mkulima wa Karanga Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma anasema kuwa ujio wa mbegu aina ya mangaka umevutia wakulima wengi walioacha kulima zao hilo kutokana na changangamoto zilizokuwa zikiwakabiri huku mbegu bora zikiwa kinzani na magonjwa na wadudu huku ikivumilia ukame.


Lengo ni tulime tupate soko na soko linahitaji bidhaa bora nzuri ambayo unalima eneo dogo lakini unapata mavuno mengi wageukie karanga zinaweza kupunguza adha ya mafuta ya kitaifa Tari wakiongeza jitihada tunaweza kuwa wakulima wa msaada kwa taifa tunayo nafasi na maeneo tunayo”


Hata hivyo Juma kafulu mkulima wakaranga kijiji cha winza alisema kuwa sasa tutafanya bishara zenye manufaa kwakulima eneo dogoo na kupata mazao mengi.


“Nimeona uwepo wa mbegu bora katika mashamba yetu uwepo wa mbegu hiyo umetuwezesha kupata mazao sana kupiitia mbegu aina ya mangaka  hata kwa sura inavutia unajua unapoweka karanga sokoni wanunuzi wengi wanaangalia mwonekano wake kasha wananunua hii mangaka itatusaidia sana katika uboreshaji wa kilimo nchini”


Mwenyekiti wa kijiji cha  Winza  Noel Ngumbi alisema kuwa uwpeo wa tafiit hizo utawasaidia sana wakulima kama wao na kuoongeza tija katika kilimo kwa nchi yetu.


“Utafiti wa karanga ulipokuja kijijini kwangu nilifarijika sana kwakuwa wananchi wangu wamekuwa wakilima karanga aina ya pongwa ambayo imekuwa ikishambuliwa sana na magonjwa na kupelekea uzalishaji kuwa mdogo hali ambayo imewapa faraja wakulima baada ya kupata mbegu ya bora kutoka tari ambayo tunaona ije kwa wingi ili kuwasadia wakulima wa kijiji hiki”


Mratibu wa zao la Karanga Kitaifa ambaye pia ni mtafiti wa zao hilo Dr Happy Daudi  alisema kuwa wanatarajia kutoa mafunzo kwa Wakulima ili kuweza kuwahamasisha kuanzisha mashamba ya mbegu za karanga ili waweze kuwauzia Wakulima wenzao.


Tunazo mbegu za majaribio lakini tunazo ambazo tayari zimeshafanyiwa utafiti na zimeanza kuonyesha Mbegu tunatoa kupitia Halmashauri yawezekana hazitoshi sasa tunawafundisha Wakulima wenzao ambapo wataweza kuipata kwa wakati na kwa urahisi kwa kiwango wanachotaka" alisema Dr Daudi


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI