Na MatukioDaimaAPP, Dar es Salaam
Juice ya miwa inayotengenezwa na taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI kituo cha Kibaha imekuwa kivutio kwa watu wangi waliobahatika kuingia katika banda la taasisi hiyo lenye bidhaa nyingi za kilimo.
Akizungumzia uwepo wa juisi hiyo Mtafiti Msaidizi kutoka Tari Kibaha Nsajigwa Mwakyusa alisema kuwa juice hiyo ya miwa inatengezwa na kuchanganya na rozela na tangawizi,
“Tunazo juice za miwa ambazo zimekuwa zikitengenezwa kituoni ambazo zimekuwa kivutio katika maonyesho ya sabasaba ina uwezo mkubwa wa kukaa bila kuwekwa kwenye jokofu ambazo zimechanganywa na rozela, tangawizi”
“Unajua hizi juice tumetengeneza kama kuwaonyesha wadau ili waongeze matumizi ya miwa nchini ambapo hata mtu asiye na meno ataweza kunywa na kuptar virubuisho stahiki”
“Zipo mbegu mbalimbali za miwa ambazo zinafaa ambapo tunazo tarisca moja na mbili zinahimili magonjwa na pia zinastahimili ukame zinakiasi kikubwa cha sukari”
“Mpaka sasa zipo mbegu sita ambazo zinafaa kwa umagiliaji kwa wenye viwanda vikubwa vya sukari ambao kwa hekta inatoa tani zaidi ya 80 zinahimili magonjwa na ukame na pia zinaviwango vikubwa vya sukari”
“Ili upate tija na tupunguze upungufu wa sukari nchini ni vema zikatumika mbegu hizi bora zinazopatikana katika kituo chetu” alisema Pamba
0 Comments