Header Ads Widget

GEREZA KWITANGA KIGOMA YAONGEZA UZALISHAJI WA CHIKICHI


Na Mwandishi wetu,


Gereza kwitanga maarufu kwa zao la chikichi mkoani kigoma limejipanga kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kuondokana na uhaba wa mafuta nchini ambapo serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.


Akizungumza wa waandishi wa habari Mkuu wa Gereza Kwitanga Uswege Mwakahesya alisema kuwa Gereza hilo lilianza kulima zao hilo katika miaka ya 60.


Alisema kuwa kutokana na miche hiyo kuzeeka wamehamasika kuanza kupanda mbegu aina ya tenera iliyofanyiwa utafiti na Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania tari kituo cha kihinga ambayo wanamatarajio makubwa ya kuongeza uzalishaji.

“Hili gereza ni maarufu kwa kilimo cha mchikichi tangia mwaka ya 1968 mpaka serikali ilipoamua kuboresha zao hili na sisi tukahamasika hadi sasa  tunayo miche 324,812 lakini tumeweza kupanda kwenye eneo la hekali 475 ambapo tumepanga miche  2375 huku tukigawa kwenye magereza mengine ikiwemo Kimbiji kwenye eneo la hekali 400 na Katavi 2200”


“Pia tumepeleka maeneo yote ambayo zao hili linakubali tutapeleka miche hii kutokea hapa lakini pia tunayo mikakati ya kuhakikisha kuwa tunaongeza eneo la upandaji wa miche mipya huku tukikata kidogo kidogo”


“Tunafurahi kwakuwa tuliambiwa kwa muda mfupi hizi mbegu zinaanza kuzaa tumeshuhudia kwenye miche tuliyopanda mwaka 2019 tukiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tayari imeshaanza kuzaa hii ni faraja tofauti na mbegu ya zamani ambayo tulikuwa tunasubiri kwa miaka mitano hadi saba.


“Hamasa hii ya kulima eneo kubwa tunarajia kuwa na kiwanda kikubwa ambacho kitasaidia na wakulima wa jirani ili kuweza kukamua mazao yao”


“Tunazo hekali 1000 zingine katika wilaya ya uvinza ambapo tutapeleka mbegu pia na tutapanda ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa chikichi ili kuweza kutatua tatizo hilo ndani ya gereza na nchi kwa ujumla”


“Sisi tunajitegemea kwa chakula naamini hata mafuta pia tutaanza kujitegemea kwenye mafuta tunaamini kuwa tutakuwa sehemu ya kuisaidia serikali kupunguza bajeti ya mafuta tunayoagiza nje ya nchi.”


“Katika miradi mingi wafungwa wanahusika kwa asilimia 100 wanajifunza kuanzia mbegu hiki ni chuo tunawafundisha na wao ndio wanahudumia mashamba haya ya michikichi” alisema Mwakahyesya


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI