Header Ads Widget

JACQUELINE MENGI ARUKA KIHUNZI CHA KWANZA MAHAKAMA YA RUFAA

 



Dar es Salaam. Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi amevuka kihunzi cha kwanza katika mapambano ya kisheria ya mirathi baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali pingamizi dhidi ya maombi yake kuhusu wosia.


Jacqueline amefungua maombi ya mapitio ya hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Mei 18, 2021 na Jaji Yose Mlyambina iliyobatilisha wosia uliokuwa unadaiwa kuandikwa na marehemu Mengi wakati wa uhai wake, ambapo anaiomba Mahakama ya Rufani ifanye mapitio ya hukumu hiyo na hatimaye ibadilishe. #JAYSADIAN___UPDATES

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI