Na Editha Karlo,Kigoma
SERIKALI ipo katika mchakato wa kupitia upya sera ya wazee ya mwaka 2003 Ili kuliwezesha kundi hilo kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi.
Katibu mkuu wizara ya afya , maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt,JOHN JINGU ametoa kauli hiyo mkoani Kigoma na kusisitiza kuwa hatua hiyo itawawezesha wazee kupata stahiki muhimu ambazo wamekuwa wakizililia kwa muda mrefu.
amesema Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine tayari imekamilisha utafiti na kuandaa rasimu ya sera hiyo na kwamba kinachosubiriwa kwa Sasa ni hatua nyingine ikiwemo suala hilo kufikishwa bungeni Ili taratibu za kutungiwa na Sheria ziendelee.
Aidha amezungumzia baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakililiwa na wazee zikiwemo posho na pensheni ya wazee na kusisitiza kuwa suala hilo tayari linashughulikiwa katika ofisi ya waziri mkuu kwa kushirikiana na wizara hiyo.
Katika kikao hicho kilichowashirikisha makatibu wakuu watatu kutoka wizara za ndani ya nchi katiba na Sheria pamoja na afya , maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto suala la kamati za MTAKUWA zinazoshughulika na utatuzi changamoto mbalimbali katika jamii limejadiliwa na kuwataka wajumbe wa kamati hizo nchini kufanya Kazi kwa moyo wa kujitolea .
Katibu mkuu Dkt,John Jingu amsema kamati hizo hazipaswi kusubiri fedha ya wadau ama serikali Ili kufanya Kazi bali zinawajibu wa kuhakikisha matitizo ama changamoto zinapotokea kwenye eneo husika zinashughulikiwa haraka bila kusubiri masuala ya fedha.
Kikao kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara tatu, Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Katba na Sheria na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kinakusudia kuanisha maeneo mbalimbali ya kijamii na kutafuta suluhisho la pamoja la changamoto zinazojitokeza.
Ziara hiyo ya Makatibu Wakuu inaendelea katika Mikoa ya Tabora, Kigoma na Kagera ikiwa ni mwendelezo wa Ziara kama hizo katika mikoa ya Mbeya, Katavi na Rukwa.
Viongozi hao wanaendelea ziara yao ya kikazi Wilayani Kibondo, Mkoani Kigoma.
0 Comments