Watu watatu, wakiwamo raia wa Msumbiji na Malawi, pamoja na Mtanzania, wamefariki dunia baada ya meli ya MV Chambo, inayofanya safari zake kati ya Tanzania na Msumbiji, kuwaka moto katika Ziwa Nyasa, mkoani Ruvuma, leo Jumapili, Oktoba 11, 2026, saa 10:30 alfajiri.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peresi Magiri, amesema meli hiyo ilikuwa ikitoka Tanzania kuelekea Msumbiji ikiwa na tani 10 za mizigo na abiria 44 wa mataifa mbalimbali.
Amesema abiria hao walikuwa raia wanne wa Malawi, 23 wa Msumbiji, 15 wa Tanzania na wawili wa Lesotho. Hii ina maana kwamba zaidi ya watu 40 waliokolewa. Ameeleza kuwa waliofariki ni mtoto wa kike, raia wa Msumbiji; mwanamke, raia wa Malawi; na Mtanzania aliyetambulika kwa jina la Yuston Chatanda, mkazi wa Njombe.
FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2027 MEDALA HIGH SCHOOL IDODI IRINGA
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 0753549368 AU 0736313160
















0 Comments