Header Ads Widget

KADHI MBEYA: MSIKITI USIWE SEHEMU YA IBADA PEKEE

 

Na Samwel Mpogole ,Matukio Daima Media Mbeya

Waumini wa Kiislamu jijini Mbeya wametakiwa kutumia misikiti kama majukwaa ya kujenga upendo, mshikamano, maelewano na amani katika jamii, badala ya kuwa sehemu za ibada pekee.

Wito huo umetolewa na Kadhi wa Mkoa wa Mbeya, Sheikh Hassan Mbarazi, wakati wa uzinduzi wa msikiti mpya katika eneo la Nsalaga jijini Mbeya.

Sheikh Mbarazi amesema misikiti ina nafasi kubwa ya kuwaunganisha watu, kujadili changamoto zinazowakabili na kutafuta suluhisho kwa pamoja.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa BAKWATA Mkoa wa Mbeya, Musa Abdala Ismail, amewapongeza wakazi wa Nsalaga kwa ushirikiano wao uliowezesha kukamilika kwa ujenzi wa msikiti huo, huku akiwataka kuutumia kama chombo cha kuimarisha amani na umoja.

Nao waumini wamesema kukamilika kwa msikiti huo kutarahisisha huduma za ibada na kuongeza mshikamano miongoni mwa wakazi wa Nsalaga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI