Header Ads Widget

MCC SALIM ASAS AUNGANA NA VIONGOZI, WANANCHI KUMUOMBEA MAREHEMU MAALIM HAFIDH AMEIR HASSAN


Na Matukio Daima Media

 MJUMBE wa kamati kuu ya chama cha Mapinduzi (MCC) Salim Asas ameungana na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Dua ya 40 ya kumwombea marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyekuwa mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dua hiyo imefanyika katika Msikiti Mkuu wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kumuombea marehemu na kuendelea kuwakutanisha viongozi, ndugu, jamaa na wananchi katika kumuenzi.


Salim Asas alishiriki katika ibada hiyo pamoja na waumini wengine waliokusanyika kwa ajili ya kumuombea marehemu, ambaye kifo chake kimewagusa watu mbalimbali kutokana na nafasi yake katika familia na jamii.


Ushiriki wa viongozi na wananchi katika dua hiyo unaonesha mshikamano wa kijamii na umuhimu wa kuwa pamoja katika kipindi cha majonzi, huku wakitoa pole na faraja kwa familia ya marehemu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI