Header Ads Widget

'NADHANI PUTIN ANATAKA MAKUBALIANO ZAIDI YA ZELENSKY' - TRUMP

Akitoa maoni yake kuhusu utekelezwaji wa mkataba wa "usitisha mapigano ya nishati" alioutangaza kati ya Urusi na ukraine, Rais wa Marekani Donald Trump alijibu: "Wao [Zelensky na Putin] walikubaliana. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu niliwaambia, 'Mnakubali.' Ndiyo maana"

Aliongeza pia kwamba kwa maoni yake, Vladimir Putin ana nia zaidi ya kufikia makubaliano kuliko Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

"Nadhani Putin anataka makubaliano zaidi ya Zelensky. Nadhani Putin anataka makubaliano, na tunahitaji kumshawishi Zelensky kutaka makubaliano," Trump alisema.

Alipoulizwa kama Urusi ilikiuka "mkataba wa kusitisha mapigano ya nishati" aliyokuwa ametangaza, Trump alijibu kwamba "kulikuwa na ukiukwaji wa sheria kwa pande zote mbili."

"Putin na Zelensky wanataka kufanya makubaliano, lakini hawajui jinsi gani. Lakini tutawalazimisha kufanya makubaliano," rais wa Marekani aliongeza.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuondoka kwenda kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa kati kati ya muhula katika jimbo la Ohio.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI