Header Ads Widget

DR. KARANJIT ATOA USHAURI KUHUSU TIBA YA MAGONJWA YA UBONGO NA UTI WA MGONGO DAR

Mkurugenzi Mwandamizi wa Idara ya Upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo katika Hospitali ya Medanta nchini India, Dkt. Karanjit Singh Narang, amewataka wananchi wenye matatizo ya ubongo, uti wa mgongo na shingo kutafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya kufikiria kufanya upasuaji au kusafiri kwenda nje ya nchi kupata matibabu.

Amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa kambi ya maalum ya matibabu iliyofanyika Septemba 11 na 12, 2026 katika Hospitali ya Tiba Healthcare Ltd iliyopo Upanga. Kambi hiyo imefanyika kwa ushirikiano na MedIncredi (Medical Travel) yenye maskani yake Ocean road Jijini Dar es salaam.

Dkt. Karanjit amewaonya wananchi dhidi ya kutafuta huduma za kuchua 'massage' au kubanwa shingo na watu wasio na utaalamu, ikiwemo vinyozi, akisema vitendo hivyo vinaweza kusababisha uharibifu wa kudumu kwenye mishipa ya fahamu na hata kupooza.

Amesema uharibifu ukitokea kwenye uti wa mgongo ni vigumu kurekebika kwa sababu seli za ubongo na uti wa mgongo hazijirekebishi kwa urahisi.

Ameongeza kuwa watu wengi wenye maumivu ya mgongo na shingo hawahitaji upasuaji. Wengi wanaweza kupata nafuu kwa kubadilisha mtindo wa maisha, kufanya mazoezi na matibabu mengine yasiyo ya upasuaji. Kwa kesi ngumu kuna teknolojia za kisasa za upasuaji wa matundu madogo.

Kwa upande wake, Dkt. Mustafa Mohamed Dadah, GP | Clinical Admin wa Tiba Healthcare Ltd, amesema katika kambi hiyo wagonjwa 70 wamehudumiwa. Siku ya kwanza walikuwa 40 na siku ya pili 30. Wengi walikuwa na maumivu ya mgongo wa chini, shingo na mabega.

Dkt. Mustafa ametoa wito kwa wananchi kutopuuza dalili kama ganzi, maumivu makali ya mgongo na shingo, na maumivu ya kichwa ya ghafla. Amesisitiza kuwa dalili hizo zinaweza kuhusiana na magonjwa kama kisukari au uvimbe wa ubongo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MedIncredi (Medical Travel), Bi. Lalita Chauhan, amesema kampuni hiyo ina mpango wa kuleta madaktari bingwa kutoka India. Pia huwasaidia wagonjwa wanaotaka kwenda kupata matibabu India pamoja na ufuatiliaji baada ya matibabu kupitia njia mbalimbali ikiwemo video call.

MedIncredi (Medical Travel) hufanya kambi kama hizo katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Tanga, Mwanza na Zanzibar, katika huduma za mifupa, meno, upasuaji wa urembo na magonjwa mengine.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI