Na Matukio Daima Media.
Wananchi wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuchukuwa hatua za mapema kwa kusafisha mitaro ya maji, mifereji na maeneo ya biashara ili kuweza kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El nino zinazotarajiwa kuanza mwezi huu Hadi machine 2027.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wananchi na wafanyabiashara alipokuwa akikagua mazingira katika Soko la Kilombero jijini Arusha ambapo amesema wataalamu wa hali ya hewa wameonesha uwezekano wa kunyesha mvua kubwa ambazo zinaweza kuzidu zile zilizowahi kushuhudiwa hapo awali.
Mhe.Reuben amesema ni muhimu kwa kila mmoja katika eneo lake kuhakikisha njia za maji zinakulwa wazi ili kuzuia mafutiko na uharibifu wa Mali ambapo amewahimiza wafanyabiashara na wananchi kushiriki kikamilifu kampeni za usafi wa mazingira huku akisisitiza kuwa kulinda mazingira na kuzibua mitaro siyo kwa manufaa ya mtu mmoja Bali ni kwa usalama wa jamii nzima, biashara na maisha ya wananchi.
Akieleza utekeleza wa dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mhe. Reuben amesema utunzaji wa mazingira ni moja ya nguzo katika utekelezaji wa dira hiyo ambapo amesisitiza upandaji wa miti kuwa sehemu ya mageuzi ya usimamizi wa mazingira na kukabiliana na athali za mabadiliko ya tabianchi.
Ameongeza kuwa serikali imelenga kufikisha matumizi ya nishati safi kwa asilimia 80 ya watanzania ifikapo mwaka 2034 ambapo amepiga marufuku magari ya serikali kubeba mkaa huku akiwataka wakuu wa mikoani, Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia kikamilifu agizo hilo.
Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuhifadhi mazingira, kupunguza ukataji wa miti na kuhakikisha Taifa linafikia malengo yake ya maendeleo endelevu.


.jpeg)
.jpeg)




0 Comments