Header Ads Widget

SAUTI MOJA 27: KANISA LA WAADVENTISTA SONGEA MJINI LAZINDUA MPANGO WA KIDIJITALI KUENEZA INJILI

Na Samwel Mpogole.

Kanisa la Waadventista Wasabato, Mtaa wa Songea Mjini, limezindua rasmi mpango wa “Sauti Moja 27” (One Voice 27), unaolenga kutumia teknolojia na majukwaa ya kidijitali kueneza ujumbe wa Injili na kuwafikia watu wengi zaidi katika jamii.

Uzinduzi wa mpango huo umefanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Songea Mjini, ukihudhuriwa na waumini kutoka Songea Mjini na Mateka.

Hafla hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista wa Sabato Nyanda za juu kusini mwa Tanzania, Toto Ndege Bwire Kusaga, ambaye amesema ujio wa mpango huo ni hatua muhimu katika kuhakikisha kanisa linatumia fursa zinazotolewa na teknolojia ya kisasa kufikisha ujumbe wa Injili kwa watu wengi zaidi.

Kwa upande wake, Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Songea Mjini, Elias Mshahara, amesema matumizi sahihi ya teknolojia na mitandao ya kijamii yanaweza kuwa nyenzo muhimu katika kuwafikia watu wa kizazi cha sasa, hususan vijana ambao kwa kiasi kikubwa hutumia majukwaa ya kidijitali katika maisha yao ya kila siku.

Mchungaji Mshahara amesisitiza umuhimu wa waumini kutumia fursa hiyo kushiriki katika kueneza ujumbe wa Injili kwa kutumia majukwaa mbalimbali ya mtandaoni.

Baadhi ya waumini walioshiriki katika uzinduzi huo wameeleza matumaini yao juu ya mpango huo, wakisema utatoa fursa kubwa zaidi kwa kanisa kufikisha ujumbe wa Injili nje ya mipaka ya majengo ya ibada na kuwafikia watu katika maeneo mbalimbali kupitia simu na mitandao ya kijamii.

Goodluck Mkosai, mmoja wa waumini walioshiriki katika hafla hiyo, amesema mpango huo una nafasi kubwa ya kupanua wigo wa uinjilisti kwa kutumia majukwaa ambayo tayari yanatumiwa na watu wengi katika jamii.

Naye Ruth Mchomvu, muumini mwingine, amesema matumizi ya teknolojia yataifanya Injili kuwafikia watu kwa urahisi zaidi, huku akiwataka waumini kutumia mitandao ya kijamii kwa maudhui yenye kujenga jamii na kueneza ujumbe wa matumaini.

Mpango wa “Sauti Moja 27” (One Voice 27) unalenga kuimarisha matumizi ya teknolojia katika shughuli za uinjilisti, kwa kuwahamasisha waumini kushiriki kikamilifu katika kutengeneza na kusambaza ujumbe wa Injili kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ya kidijitali.

Mpango huo unakuja wakati ambapo matumizi ya teknolojia yamekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku, hususan kwa vijana, hivyo kutoa fursa kwa kanisa kutumia majukwaa hayo kufikisha ujumbe wa kiroho kwa hadhira pana zaidi.

MWISHO 

KUPIGA KURA ZA SAMIA KALAMU AWARDS KWA MATUKIO DAIMA MEDIA INGIA HAPA 


MATUKIO DAIMA MEDIA IMETEULIWA KUWANIA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026 ILI KUSHINDA TUZO HIZO INAHITAJIKA KURA ZA WANANCHI ZA KUTOSHA HIVYO TUNAOMBA KURA YAKO KUPIGA KURA BONYEZA LINK HII CHINI KISHA UTAONA SEHEMU IMEANDIKWA KURA KURA UTABONYEZA NA MWISHO SEHEMU IMEANDIKWA NDIO UTAKUWA UMEPIGA KURA UTAFANYA HIVYO KWA TUZO YA KWANZA HADI YA NNE.

⬇️⬇️⬇️BONYEZA HAPA 
KUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ISHINDE TUZO ZA SKA 2026 INGIA HAPA KIRAHISI ZAIDI
 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI