Header Ads Widget

WANACHAMA SIMBA TAWI LA WAFANYABIASHARA MAFINGA WAMZIKA MWANACHAMA MWENZAO MERIRIAN MTISI

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, MAFINGA


WANACHAMA wa Simba Tawi la Wafanyabiashara wa Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, wameungana na mamia ya waombolezaji wa Mji wa Mafinga katika mazishi ya mwanachama mwenzao, Marehemu Meririan Damian Mtisi, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na ndugu, jamaa, marafiki, wafanyabiashara pamoja na wanachama wa Simba ambao walijitokeza kwa wingi kutoa heshima zao za mwisho na kumsindikiza mwenzao katika safari yake ya mwisho.



Akizungumza na Matukio Daima Media, Methew Mkumbo Meriana Mtisi alikuwa mjumbe kamati tendaji hivyo aliwashukuru wanachama wa Simba pamoja na wananchi wote waliojitokeza kushiriki katika mazishi hayo, akisema ushiriki wao umeonesha upendo, mshikamano na umoja katika kipindi hicho kigumu cha kuondokewa na mwenzao.

Mkumbo alisema Marehemu Mtisi alikuwa mwanachama mwenzao ambaye katika kipindi cha uhai wake alitoa mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali, hivyo wataendelea kukumbuka na kuuenzi mchango wake.

Alisema wanachama wa Simba Tawi la Wafanyabiashara Mafinga wanatambua nafasi aliyokuwa nayo marehemu miongoni mwao na kwamba kifo chake kimeacha pengo kwa familia, ndugu, marafiki na wanachama wenzake.

Aidha, Mkumbo ametoa wito kwa wana Simba kuendelea kudumisha mshikamano, upendo na kusaidiana katika nyakati za furaha na huzuni, akisisitiza kuwa umoja huo ni muhimu katika kuimarisha mahusiano miongoni mwa wanachama.
Alisema kujitokeza kwa wanachama na wananchi katika mazishi hayo ni ishara ya namna jamii ilivyoguswa na msiba huo na kuthamini maisha na mchango wa Marehemu Mtisi wakati wa uhai wake.

Ndugu, jamaa na marafiki nao waliungana kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu huku wakimuombea apumzike kwa amani.


Kwa mujibu wa taarifa za marehemu, Meririan Damian Mtisi alizaliwa Desemba 3, 1985 na kufariki dunia Septemba 7, 2026.

Wanachama wa Simba Tawi la Wafanyabiashara Mafinga wameendelea kutoa pole kwa familia, ndugu na wote walioguswa na msiba huo.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Meririan Damian Mtisi mahali pema peponi. Amina.





 MAGAZETINI LEO ALHAMISI SEPT 10/2026:HATUA KWA HATUA KESI YA KUTEKA WAKWE ZAKE . | https://www.matukiodaimamedia.co.tz/2026/09/magazetini-leo-alhamisi-sept.html




KUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ILI KUSHINDA TUZO YA SKA2026 BONYEZA LINK HII 


⬇️

BONYEZA HAPA KUPIGA KURA ZOTE NNE

FUNGUA KISHA PIGA KURA YA KWANZA YA CHOMBO PIGA KURA YA PILI HADI YA 4 KILA BAADA YA MASAA 24 HADI SEPT 30


AHSANTE KWA KUIPA NGUVU YA USHINDI MATUKIO DAIMA🙏🙏🙏

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI