![]() |
| Tawi la Wekundu wa Ngorongoro Kreta wakipaisha bendera ya destination Ngorongoro na kutangaza vivutio vya utalii |
Wakati Klabu ya Simba ikihitimisha kwa kushindo wiki ya mnyama tarehe 8 Agosti, 2026 Dar es Salaam, Ngorongoro kupitia tawi la Wekundu wa Ngorongoro Kreta walipaisha bendera ya destination Ngorongoro na kutangaza vivutio vya utalii katilka tamasha hilo lililokutanisha maelefu wa watazamaji wa ndani na nje ya nchi.
Maelfu ya mashabiki wa Simba waliokusanyika katika tukio hilo walipata fursa ya kufahamu zaidi kuhusu vivutio vya utalii vinavyopatikana Ngorongoro, huku wanachama wa tawi hilo wakisisitiza umuhimu wa kutumia nguvu ya mashabiki wa michezo kama jukwaa la kufikisha ujumbe wa utalii kwa jamii.
Kwa Tawi la Wekundu wa Msimbazi Ngorongoro Crater, ushiriki wao haukuwa tu kwa ajili ya kuunga mkono timu yao pendwa, bali pia ulikuwa sehemu ya juhudi za kuunganisha michezo, utamaduni wa ushabiki na utalii katika kuhamasisha Watanzania kutembelea vivutio vya ndani.
Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa Tawi la Wekundu wa Msimbazi Ngorongoro Crater, Ndugu Herbert Mdome, alisema ushiriki wao katika Simba Day ulikuwa na malengo mawili makubwa ambayo ni kuunga mkono klabu yao na kutumia jukwaa hilo kuitangaza Ngorongoro.
“Chapa kubwa za Ngorongoro na Simba zimeungana, Sisi kama tawi tumekuja Simba Day kuunga mkono timu yetu na kutumia jukwaa hili lenye mamilioni ya watazamaji duniani kote kutangaza maajabu ya vivutio vilivyopo Ngorongoro na kuwahakikishia mashabiki wote kuwa Ngorongoro ndio nyumbani kwa kila binadamu
,” alisema Mdome
Kwa upande wake, Mtunza Hazina wa tawi hilo, Faudhi Seleman , alisema utambulisho wao unaunganisha mapenzi kwa klabu hiyo na uzalendo katika kuitangaza Ngorongoro kama Premium Safari Destination Ngorongoro
Ushiriki wa Tawi la Wekundu wa Msimbazi Ngorongoro Crater unaonyesha namna ambavyo taasisi na wadau wa utalii wanaweza kutumia majukwaa yenye ushawishi mkubwa katika jamii, ikiwemo michezo na mashabiki, kufikisha ujumbe wa utalii kwa hadhira pana kote ulimwenguni.











0 Comments