Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, naomba niwaage rasmi wajumbe wenzangu wa Kamati Tendaji ya Kanda ya Nyasa
Leo tarehe 8/8/2026 nimewasilisha rasmi barua yangu ya kujiuzulu kwa Katibu wa Kanda Grace Shio.
Ikumbukwe kuwa nimekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Kanda ya Nyasa kwa awamu ya pili. Katika uongozi wa Kanda uliomaliza muda wake chini ya Mwenyekiti Mstaafu Peter Simon Msigwa mimi pia nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uenezi ya Kanda kwa awamu yote. Hivyo, huu ulikuwa pia wakati wangu wa pili wa kuitumikia nafasi hiyo.
Kwa moyo wa dhati, napenda kutoa shukrani nyingi sana kwa wanachama na viongozi wote wa mikoa mitano — *Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa*— kwa ushirikiano mkubwa mlionipa wakati wote wa uongozi wangu. Bila nyinyi, safari hii isingekuwa rahisi.
Kwa namna ya pekee, napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa sasa wa Kanda ya Nyasa, Ndugu,*Mh.Joseph O. Mbilinyi (Sugu)*, kwa uongozi wake, ushirikiano na nafasi niliyopata ya kuendelea kukitumikia chama katika kipindi hiki. Nathamini sana ushirikiano tuliokuwa nao na ninamtakia kila la heri katika kuiongoza Kanda yetu.
Nimejiuzulu nafasi ya uongozi, si uanachama wa chama. Nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu na kushiriki katika mapambano kadiri nitakavyoweza. Kwa sasa, naombeni nipumzike na nijielekeze zaidi kwenye afya yangu.
Nawaaga kwa nafasi hii, lakini siondoki kwenye mapambano. Tutakutana wakati mwingine, Mungu akitoa nafasi tena.
Kwa viongozi na wanachama wenzangu, tuendelee kukipigania chama chetu, tuendelee kuwa na imani na viongozi wetu wa kila ngazi, na tuunge mkono kila hatua inayolenga kukijenga chama chetu — bila kuchoka wala kukata tamaa.
Asanteni kwa kila kitu. Mungu awabariki sana.
Bruce Cuthbert Nyamwangi
Mnyakwibata
Bepari Mnyalu
PEOPLESSSSSSSSSSS — MAPAMBANO YANAENDELEA!








0 Comments