Header Ads Widget

DKT. SIMBEYE ASISITIZA UMOJA WA VYUO VYA UALIMU KULETA MAPINDUZI YA ELIMU


 

Na Matukio Daima Media Dodoma

SERIKALI imesisitiza kuwa ubora wa walimu wanaoandaliwa katika vyuo vya ualimu ndio utakaoamua mustakabali wa elimu nchini katika miaka ijayo.

Akifungua kikaokazi cha Wakuu wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali pamoja na Waratibu wa Taaluma jijini Dodoma, Agosti 6, 2026, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule, Dkt. Ephraim Simbeye, amewataka Wakuu wa vyuo kuimarisha usimamizi wa mafunzo ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa na umahiri, maadili na stadi zinazokidhi mahitaji ya Taifa.


Ameongeza kuwa vyuo vya Ualimu vina jukumu kubwa katika utekelezaji wa mtaala kwa kuhakikisha walimu wanaohitimu wanakidhi viwango hitajika.

Dkt. Simbeye ameeleza kuwa kikaokazi hicho kimefanyika katika kipindi muafaka baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa wahitimu wa Mtaala Ulioboreshwa wa Elimu ya Ualimu ulioanza kutekelezwa mwaka 2023 na kusema kuwa hatua hiyo inatoa nafasi ya kutathmini mafanikio, changamoto na maeneo yanayohitaji maboresho.

Kiongozi huyo amesema kuwa Wakuu wa Vyuo wanapaswa kuwa wabunifu katika matumizi ya rasilimali. Ushirikiano na sekta binafsi pamoja na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali bila kuathiri utoaji wa elimu.


Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia miongozo ya Serikali katika utekelezaji wa mtaala, mafunzo kwa vitendo na utoaji wa mafunzo kwa njia ya masafa, ili kuhakikisha nchi inapata walimu wenye viwango vinavyofanana vya umahiri, maadili na uzalendo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu ya Ualimu na Mafunzo, Mathias Mvula, amesema lengo la kikao kazi hicho ni kubadilishana uzoefu uliopatikana katika utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa wa Elimu ya Ualimu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI