.Linatarajia kuwakutanisha watu 8,000 mkoani Mara
Na Matukio Daima Media, Dodoma.
SHIRIKA la Vi Agroforestry linatarajia kufanya kongamano kubwa la kilimo misitu kwa vijana linalotarajia kufanyika Mkoani Mara mwezi Oktoba mwaka huu likitarajiwa kushirikisha zaidi ya watu 8,000.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkaazi wa shirika hilo, Martha Olotu katika kongamano la wadau wa kilimo lililofanyika katika maonesho ya nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Malechela Nzuguni Jijini Dodoma.
Alisema wameamua kujikita katika vijana kwa kualika vijana wengi kushiriki kongamano hilo kwani wanatambua kuwa katika upande huo kuna fursa nyingi na vijana ndio nguvu kazi ya Taifa.
Alisema mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Vijana Joel Nanauka ambaye ataongea na vijana uso kwa usona kuwaeleza fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye kilimo misitu.
Martha alisema Shirika lina miaka 30 tangu lianze kufanyakazi hapa nchini na lilianza kufanya kazi mkoa wa Mara na ndipo baada ya hapo wakaenda kufanya kazi kwenye mikoa mingine ya Dodoma, Manyara, Lindi, Mtwara na Kagera.
Alisema Shirika hilo linaongozwa na Mpango mkakati wa miaka mitatu ambao unatarajiwa kukamilika mwaka 2027 na kuongeza kuwa wanatarajia kuwa na mpango mkakati mwingine ambao utaanzia 2028 kwneda mbele.
Alisema shirika linatekeleza miradi mbalimbali na linawadau wa aina tatu ambao ni shirika la wakulima wadogo asasi za kiraia ambazo zinawajenga uwezo mashirika ya wakulima na kuchukua mahitaji kutoka kwa wakulima hao kupeleka kwa wafanya maamuzi.
Alisema shirika hilo linaongozwa na program maalum ambayo inazingatia sana uwindaji unaozingatia baionua na mabadiliko ya tabia nchi.
“Leo tulikuwa na kikao maalum kuangalia shirika hili limefanyakazi gani tumeangalia bajeti ya Wizara ya Kilimo na bajeti ya utalii ambazo zilisomwa kwenye bajeti ya serikali, tuliangalia mapungufu yaliyomo kwenye bajeti zile na kuishauri serikali namna ya kufanya kuondoa mambo ambayo tumeona ni changamoto,” alisema
“Tumeishauri serikali kuhusu masuala mbalimbali ambayo tunaona yanafaaa kufanyiwa marekebisho na tumeangalia fursa zilizomo kwenye bajeti hiyo na sisi tunatarajia kuanzisha mtandao wa mashirika yanayofanyakazi za kilimomisitu na tumekaribisha watu wajisajili ,” alisema Olotu
“Kwenye kongamano la mwaka huu tunatarajia kuwa na washiriki 8,000 mwaka jana walikuwa 6,000 ila mwaka huu wataongezeka mpaka sasa tunawashiriki 3,000 wameshajisajili kwaajili ya kushiriki kongamano hilo, tunafanyamakongamano Mara kwasababu tulianzia kazi Mkoa wa Mara kwa hiyo mkoa wa Mara ni nyumbani,” alisema Martha
Naye Edna Paul kutoka Shirika la Counsenult alisema kuwa kilimo misitu inavyoweza kuchangia kuelewa athari za mabadiliko ya tabia ya inchi kutunza udongo lakini kupitia mazao inaweza kukabiliana na tatizo la utapiamlo kama chakula kitapatikana cha kutosha.
Alisema kuwa watakaoshiriki katika kongamano hilo watapata fursa ya kujifunza masuala ya kilimo misitu na mabadiliko ya tabia inchi itakayowasadia kufanya kilimo chenye tija na kupata chakula cha kutosha na kutokomeza kabisa utapiamlo.
Aidha Nemesi Kiliya, ambaye ni Mkurugenzi wa Civil Social Protective Foundation ambao ni wabia wa Vi Agroforestry alisema kuwa wanatarajia kuanzisha jukwaa la wadau wa kilimo litakalozinduliwa na Waziri wa Vijana, Joe Nananuka.
Mwisho












0 Comments