Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeanza kutekeleza ahadi ya kurejesha ardhi ya misitu iliyoharibiwa kwa kiwango kikubwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha ardhi inaendelea kuwa hai na yenye uwezo wa kuhimili mifumo ya ikolojia kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Akizungumza katika kikao kazi cha kujadili Mradi wa Urejeshaji endelevu wa Mazingira na Uhifadhi wa Bayonuai, Naibu Katibu Mkuu Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Mitawa, amesisitiza umuhimu wa kutunza mazingira, akieleza kuwa ardhi ndiyo msingi wa maisha na nguzo muhimu ya maendeleo endelevu.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Vyanzo vya Mbegu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Dkt. Fortunata Senya, amesema ushirikishwaji wa wadau, taasisi na mashirika mbalimbali ni nguzo muhimu katika kuhakikisha lengo la kurejesha ardhi iliyoharibiwa linafikiwa kwa ufanisi na kwa matokeo endelevu.
Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mbegu za Miti wa TFS, Dkt. Hamza Katety, amesema kikao kazi hicho kinatarajiwa kutoa majawabu na mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha utekelezaji wa mpango wa urejeshaji wa ardhi ya misitu na kuhifadhi bayonuai nchini.















0 Comments