Header Ads Widget

BUNDI LATUA CHADEMA HECHE KAMA SALIMU MWALIMU WA CHAUMA

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia, ambayo ilikaa na kumaliza kikao chake juzi mjini Kigoma, ilijikuta ikimuelekezea Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa tuhuma mbalimbali zilizotolewa na wajumbe wa kikao hicho.

1. Tuhuma za Godbless Lema

Kwa mujibu wa taarifa ya mwandani wetu, Mh. Godbless Lema ndiye aliyefungua mjadala kwa kueleza mbele ya Mwenyekiti kuwa Makamu Mwenyekiti amekuwa akichukua fedha kutoka kwa wadau bila kuziwasilisha chamani.

Lema alitoa mfano wa shilingi milioni 60 ambazo alimkutanisha Makamu Mwenyekiti na mdau. Baada ya fedha hizo kuchukuliwa, hakuna hata senti moja iliyowasilishwa kwenye chama. Makamu Mwenyekiti alikiri kupokea fedha hizo na kudai alidhani alikuwa amepewa binafsi, si kwa ajili ya chama.

Lema pia alimtuhumu Makamu Mwenyekiti kwa ubinafsi na kujitengenezea utukufu wakati Mwenyekiti akiwa gerezani. Alidai kuwa Makamu Mwenyekiti alikwenda Ruvuma na kukubali kuvikwa uchifu, jambo alilolitafsiri kama tamaa ya madaraka na ubinafsi. Aidha, alidai Makamu Mwenyekiti hataki Mwenyekiti atoke gerezani kwa sababu anaendelea kupata michango kwa manufaa ya familia yake.

Lema aliongeza kuwa wakati Makamu Mwenyekiti alipokuwa akihusishwa na kesi ya uhaini, alimtuma kaka yake Chacha pamoja na Manchali kwenda kuzungumza na Serikali ili suala hilo limalizike. Hata hivyo, kwa upande wa kesi ya Lissu, alidai Makamu Mwenyekiti hakutaka kukutana na Serikali. Mwishoni, Lema alimtuhumu kuwa amekuwa akiiba michango ya chama.

2. Tuhuma za Joseph Mbilinyi (Sugu)

Mh. Sugu alieleza kuwa Makamu Mwenyekiti alipokea shilingi milioni 10 kutoka kwa mdau. 

Baada ya kuuliza kwa Katibu Mkuu, alibaini fedha hizo hazikuwa zimewasilishwa chamani.

Sugu alisema alimfuata Makamu Mwenyekiti na kumweleza kuwa kama fedha hizo haziwasilishwi chamani, basi yeye alipwe asilimia 10, ndipo Makamu Mwenyekiti akamtumia shilingi milioni 1.

Mbele ya Kamati Kuu, Makamu Mwenyekiti alikiri tukio hilo, lakini akasema alidhani mchango huo ulikuwa wa binafsi.

3. Tuhuma za Leonard Magere

Ndugu Leonard Magere alitoa ushahidi kuwa Makamu Mwenyekiti alipokea shilingi milioni 20 kutoka kwa mfanyabiashara wa madini na hakuzifikisha chamani.

Magere pia alidai aliombwa apokee shilingi milioni 1 kama kifuta jasho ili akae kimya. Makamu Mwenyekiti alikanusha kumhonga Magere, lakini alikiri kupokea shilingi milioni 20 kutoka kwa mdau wa madini.

4. Tuhuma za Boniyai

Boniyai naye alitoa tuhuma kuwa Makamu Mwenyekiti alipokea shilingi milioni 40 kutoka kwa mdau, fedha ambazo nazo hazikuwasilishwa kwenye chama.

Majibu ya Makamu Mwenyekiti

Baada ya tuhuma zote kutolewa, Makamu Mwenyekiti alilazimika kuwa mpole kwa kuwa hakuwa na utetezi wa kina. Katika maelezo yake, alikiri kupokea baadhi ya fedha zilizotajwa, lakini akasisitiza kuwa alidhani zilikuwa michango ya binafsi na si ya chama.

Msimamo wa Katibu Mkuu na Maamuzi ya Kamati Kuu

Katibu Mkuu John Mnyika alisimama na kutoa mwelekeo uliosaidia kuzuia hatua zaidi dhidi ya Makamu Mwenyekiti.

Kamati Kuu ilifikia maamuzi yafuatayo:

1. Ilieleza kuwa si maadili ya kiongozi kuchukua fedha za chama na kuzitumia bila kuziwasilisha kwenye chama. Hivyo, Kamati Kuu ilitoa onyo kwa Makamu Mwenyekiti kuhusu kukusanya na kutumia fedha za chama bila utaratibu.

2. Kamati Kuu iliunda timu ya maridhiano itakayoongozwa na Godbless Lema. Timu hiyo haitatangazwa hadharani, lakini itahakikisha inakutana na Serikali kwa ajili ya kushughulikia kesi ya Mh. Lissu ili atoke gerezani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI