Na Matukio Daima, Dar es Salaam
Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba anatarajia kesho kuzindua kitabu Cha 'Falsafa ya Sheria ya Mama Samia' kilichoandaliwa na Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA).
Makamu wa Rais wa TPBA, Debora Mchalo aliwaeleza waandishi wa habari mapema leo Julai 9, 2026 kwamba kitabu hicho kimeandaliwa kwa lengo la kuelezea kwa kina, kwa ushahidi na takwimu, namna sheria mbalimbali zilizotungwa nchini zilivyochangia kuleta mafanikio makubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
"kutokana na wingi wa sheria zilizopo nchini, waandishi wa kitabu waliamua kujikita katika uchambuzi wa sheria zilizotungwa kuanzia mwaka 2021, kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na ndio maana wakakipa jina la Falsafa ya Sheria ya Mama Samia.
"Kitabu hicho kinachambua mageuzi makubwa ya kisheria yaliyofanyika tangu mwaka 2021 hadi sasa, yakihusisha sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji, kodi, elimu ya juu, ardhi, nishati na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,"amesema Makamu wa Rais Mchalo.
Akifafanua zaidi alisema uchambuzi wa kina katika kitabu hicho umefanywa na mawakili waliobobea katika taaluma ya sheria, kwa lengo la kuweka kumbukumbu ya mchango wa mageuzi ya kisheria katika kuimarisha utawala bora na kuchochea maendeleo ya Taifa.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa alisema TPBA kinatarajiwa
kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka, utakaowakutanisha wanachama kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya taaluma ya sheria, utendaji wa chama na mchango wa mawakili wa serikali katika kuimarisha utoaji wa haki nchini.
Alisema kitabu hicho kinaeleza namna maboresho ya kisheria yalivyowezesha maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji, nishati, mawasiliano, habari na maeneo mengine muhimu ya uchumi.
Said alisema maendeleo ya nchi yoyote hayawezi kupatikana bila kuwa na mfumo madhubuti wa sheria zinazotungwa na kutekelezwa kwa ufanisi, ndiyo maana mawakili wa serikali kupitia chama chao waliamua kukusanya na kuandika mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa Rashid, kitabu hicho hakijajikita katika uchambuzi wa sheria pekee, bali pia kinaangazia sera na maamuzi ya kimkakati yaliyowezesha Tanzania kupata mafanikio katika nyanja za uchumi na ustawi wa jamii.
Mbali na Waziri Mkuu, Mawaziri wengine 10 wamethibitosha kushiriki uzinduzi huo.
Mwisho






0 Comments