NA JOSEA SINKALA, MBEYA DC.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imefanikiwa kukusanya mapato ya ndani shilingi bilioni 7.9 sawa na asilimia 101, ikiwa ni zaidi ya asilimia 100 ya mapato yaliyokadiriwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ambayo ililenga kukusanya shilingi bilioni 7.8.
Mapato yaliyokusanywa yanajumuisha vyanzo halisi vya mapato ya ndani katika shughuli muhimu za kiuchumi na kijamii ikiwemo biashara, viwanda na uwekezaji, fedha na uhasibu, sheria, kilimo mifugo na uvuvi, maliasili, afya na ustawi wa jamii, mazingira na usafi, ujenzi na miundombinu, pamoja na utamaduni na sanaa.
Makusanyo ya mapato hayo yana jumuishi pia ukusanyaji wa mapato fungwa (protected sources) ikiwemo Bima ya Mfuko wa Jamii (iCHF) Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, mapato ya papo kwa papo (user fee), kodi ya majengo na michango ya jamii katika ngazi ya vijiji na kata.
Akizungumza wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji robo ya tatu kipindi cha Januari mpaka Machi 2026 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bi. Aidda Haule, amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ina maeneo tisa (9) yanayochangia moja kwa moja kwenye mapato ya Halmashauri.
Mhe. Aida amesema katika eneo la biashara, viwanda, uwekezaji Halmashauri imekusanya zaidi mapato kupitia ushuru wa leseni za biashara kwa kiwango cha asilimia 118 sawa na shilingi milioni 228, ikiwa ni juu zaidi ya makadirio ya bajeti, ambapo Halmashauri ilikadiria kukusanya kiasi cha shilingi milioni 194.
“Eneo hili limekusanya jumla ya shilingi milioni 248 sawa na asilimia 92 mpaka kufikia tarehe 30 Aprili 2026 kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo ushuru wa nyumba za wageni asilimia 22; ushuru wa leseni za vileo asilimia 38, ada ya uwakala wa LATRA asilimia na ada za usajili asilimia 66”, ameeleza Mwenyekiti wa Halmashauri.
Mwenyekiti Aidda ameeleza zaidi kuwa eneo la fedha na uhasibu limeongoza kwa ukusanyaji wa mapato kutoka katika ada ya upangishaji wa vyumba, ambapo shilingi milioni 178 sawa na asilimia 86.
Ameeleza ushuru wa huduma umechangia kiasi cha shilingi milioni 678 sawa na asilimia 85; ushuru wa magulio shilingi milioni 16 sawa na asilimia 40; ushuru wa maegesho na stendi shilingi 119 sawa na asilimia 67 na ushuru wa soko shilingi milioni 36 sawa na asilimia 67.
Katika eneo la kilimo, mifugo na uvuvi, Mwenyekiti amesema Halmashauri imekusanya mapato zaidi kutoka katika ushuru wa zao la parachichi shilingi milioni 42.6 sawa na asilimia 142 ya makadirio ya bajeti. Pia zao la kahawa limefuatia katika ukusanyaji wa mapato ya shilingi 846.6 sawa na asilimia 130 ya makadirio ya bajeti.
“Ushuru wa Pareto umekusanya shilingi milioni 205 sawa na asilimia 70 maharage shilingi milioni 48.2 sawa na asilimia 47; ushuru wa mahindi shilingi milioni 237.6 sawa na asilimia 99 ushuru wa mchele shilingi milioni 4.5 sawa na asilimia 11 ushuru wa ndizi shilingi 842,000/ sawa na asilimia 17..








0 Comments