Mtu mmoja amefariki dunia huku wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya ajali ya barabarani iliyohusisha fuso kufeli breki na kugonga , daladala ,magari kadhaa , bajaji na pikipiki katika eneo la Mlima Ipogoro, Manispaa ya Iringa.
Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 7 mchana baada ya fuso hilo lililokuwa likitokea katikati ya Mji wa Iringa kuelekea Ipogoro kudaiwa kufeli breki na kuyagonga magari mawili na bajaji.
Daladala iliyohusika katika ajali hiyo ni aina ya Toyota Hiace, inayofanya safari za abiria kati ya Mji wa Iringa na Viwengi, Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema fiso hilo lilishindwa kusimama baada ya kufeli breki na kugonga kwanza bajaji kabla ya kuigonga daladala, hali iliyosababisha taharuki kubwa miongoni mwa abiria na wananchi waliokuwa eneo la tukio.
TAZAMA VIDEO YA AJALI BOFYA LINK HII
Licha ya magari hayo kupata uharibifu, taarifa za awali zinaeleza kuwa mwanamke mmoja mfanyabiashara wa mitumba amefariki dunia huku watu kadhaa wakipata majeraha na kukimbizwa hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ,jitihada za kumpata kamanda wa polisi mkoa wa Iringa zinafanyika ili kupata taarifa zaidi









0 Comments