Header Ads Widget

MIAKA 20 YA SIKU YA MATENDO MEMA: VIJANA ZAIDI YA 700 DAR WATAKIWA KUJENGA UWEZO

Picha ya pamoja  Aprili 18,2026


Na. Mwandishi Wetu, Dar.

MAADHIMISHO ya miaka 20 ya Siku ya Matendo Mema (Good Deeds Day) Nchini yamefanyika Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Don Bosco, Oysterbay, Tukio hilo limewakutanisha vijana zaidi ya 700 na taasisi 40 kwa ajili ya Elimu, burudani, na kujifunza namna ya kubadili matendo mema kuwa mifumo endelevu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee, alisisitiza kuwa kipimo cha mtu sio cheo au pesa, bali Uwezo.

"Uwezo wa kufikiri, kudhibiti hisia, na kujijenga ndio unaojenga mustakabali. Sio wengi wanaotenda mema, inahitaji ujasiri, muhimu ni kujenga uwezo," amesema Murtaza.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee, akitoa neno April 18, 2026


Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee (kulia) akitoa cheti cha Shukrani kwa mshiriki (mwenye kofia) wa kongamano hilo, April 18,2026

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee, akiwa na Kiongozi wa Good Deeds Day Tanzania, Bi. Doroth Namuhisa katika picha ya pamoja, Aprili 18,2026

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee, akitembelea wadau washiriki,  April 18, 2026


Ameongeza kuwa, Uwezo wa msingi huanza utotoni na huwajenga vijana kuendelea kuchangia jamii bila kukata tamaa.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Good Deeds Day Tanzania, Bi. Doroth Namuhisa, amesema mwaka huu harakati zinaongozwa na kauli mbiu "Tuungane pamoja katika kufanya matendo mema kutoka moyoni". Lengo ni kuhimiza watu kutenda mema kwa hiari, kwa kutumia muda, ujuzi na maarifa waliyonavyo.

"Tunasisitiza fikiri wema. Ukifikiria mema, utazungumza mema na hatimaye utatenda mema. Dunia inaweza kuwa salama zaidi endapo kila mmoja atachukua jukumu," amesema Doroth.

Kiongozi wa Good Deeds Day Tanzania, Bi. Doroth Namuhisa akimkabidhi cheti cha Shukrani mmoja wa washiriki wa kongamano hilo la miaka 20 ya Siku ya Matendo mema, April 18, 2026.

Kiongozi wa Good Deeds Day Tanzania, Bi. Doroth Namuhisa akizungumza katika kongamano hilo la miaka 20 ya Siku ya Matendo mema, Aprili 18,2026



Good Deeds Day huadhimishwa kila Aprili na inachangia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) kupitia uhifadhi wa mazingira, afya, elimu, usawa wa kijinsia na kupunguza umaskini.

Baadhi ya wadau na taasisi na mashrika ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali yaliyoshiriki ni pamoja: UTT AMIS, Dar City promotions, Coca Cola.

Wengine: Natalia Foundation, Rotaract, Mega We Care, PGN Career Solutions, Young life Tanzania, Mental Health Africa, Builders of Future, ⁠Sana Mare. One Health Society, Ingu group, Jenga Wellness Hub,  ⁠Fahari Tuamke Maendeleo, Afya Connect Digital Doctors, ⁠Lupus Tanzania Organisation, ⁠Youth Voice Organization na wengineo.

Kiongozi wa Good Deeds Day Tanzania, Bi. Doroth Namuhisa akikabidhiwa mti na kitabu kutoka kwa washiriki wa kongamano hilo la miaka 20 ya Siku ya Matendo mema, April 18, 2026




































Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI