Header Ads Widget

MAGAZETINI LEO JUMATATU APRIL 20/2026: VUNJABEI AUCHUNGULIA UBUNGE ISIMANI


 

Matokeo ya Kura za Maoni Ubunge Jimbo la Ismani 2026: 


Fredy Vunjabei Aongoza kwa Kishindo Matokeo ya kura za maoni ndani ya chama chama cha Mapinduzi (CCM) yametangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi huo mdogo ndani ya CCM Sule Masanguti,kuwa aliyeongoza ni Fredy Fabian Ngajiro maarufu kama Vunjabei .

 Vunjabei ameibuka kinara kwa jumla ya 2,703, akifuatiwa  Festo Shemu Kiswaga akipata kura 868,huku  Emmanuela Kaganda Mtatifikolo akipata kura 682 na Arif Abri kura 233.

Akitangaza matokeo hayo  Masanguti alisema jumla ya wanaccm 18 ndio waliojitokeza kuchukua fomu na wote walirejesha na kuwa  Dkt Abdalah Lusasi alipata  kura 100,Claudia Francis (69), Asakwe Widambe (58) Elias Kazikuboma (52), Eng Sebastian Kiyoyo( 37) , Josephat Masambwa (34), David Komba( 27), Tedson Ngwale (24), Egidy Mkolwe (23),Watende Kiyagi (16) , Dkt Tumain Msowoya ( 15), Lazaro Francis Gwira(10), Thitho Cholobi (9), na Thobias Mwilapwa(5). 

Alisema huo ni matokeo hayo ni ya awali na mchakato wa vikao ndani ya chama unaendelea.


 Matokeo hayo yanaonyesha ushindani mkubwa uliokuwepo katika mchakato huo wa kura za maoni, huku wagombea zaidi ya 18 wakishiriki kuwania nafasi hiyo. 

 Hata hivyo, Vunjabei ameonyesha nguvu kubwa ya kisiasa kwa kuongoza katika kata nyingi, akiwemo kushinda kwa tofauti kubwa katika maeneo yote hadi kata wanazotoka wapinzani wake .

 Matokeo haya ya kura za maoni yanaweka mwelekeo wa nani anayeweza kupewa ridhaa ya chama kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao japo bado vikao vya juu vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho . 


 Wakizungumza baada ya matokeo hayo kutangazwa baadhi ya wana CCM waliotia nia Dkt Tumain Msowoya ,Arif Abri na Lazaro Francis Wamepongeza mchakato huo ndani ya chama . 

CCM wameanza mchakato huo wa ndani wa kura za maoni kuelekea uchaguzi mdogo wa jimbo hilo la Ismani kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Wiliam Vangimbe Lukuvi .

Hata hivyo watia nia wenzake Arif Abri ,Dkt Tumain Msowoya na Dkt Lazaro Francis wamepongeza mchakato huo kuwa umekwenda vizuri na wapo tayari kuungana nae iwapo chama kitarejesha jina lake.


Vunjabei imeweza kukaribia nyayo za Lukuvi kukubarika na wapiga kura wa Isimani kwa kupata kura pande zote za jimbo hadi kwenye kata na tarafa wanazotoka wagombea wenzake .

Ikumbukwe wakati wa kura za maoni CCM  mwaka jana 2025 ,Lukuvi amepata jumla ya kura 5,746 huku mpinzani wake wa karibu, Festo Kiswaga, akipata kura 1,159  wakati leo Vunjabei akifuata kwa kukubarika kwa kupata kura 2,703, akifuatiwa  Festo Shemu Kiswaga akipata kura 868,huku  Emmanuela Kaganda Mtatifikolo akipata kura 682 na Arif Abri kura 233.


 TAZAMA FULL VIDEO KUPITIA YOUTIBE( MATUKIO DAIMA TV) KUTANGAZA NASI PIGA SIMU 0754026299 UWAPO MJINI IRINGA

 KARIBU CLOCK TOWER CAFE PIGA SIMU 0677220022 clock tower cafe Home of Delicious Meals

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI