Header Ads Widget

IRGC IKO 'TAYARI KUMTII KIKAMILIFU' KIONGOZI MPYA MKUU - VYOMBO VYA HABARI VYA IRAN

 

Shirika la Utangazaji la serikali ya Iran (Irib) na shirika la habari la Tasnim, linaloungwa mkono na IRGC, yote yametoa taarifa iliyotolewa kwa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kukaribisha uteuzi wa Mojtaba Khamenei.

Taarifa hiyo inamuelezea Khamenei kama "mwanasheria mwenye ujuzi, mtaalamu na mwenye ufahamu mzuri zaidi katika masuala ya kisiasa na kijamii".

Jeshi la Iran( IRGC) pia limetangaza "kuheshima, kujitolea na kutii" kiongozi wake mpya Khamenei, likisema kwamba wanachama wake "wako tayari kumtii kikamilifu na kujitolea katika kutekeleza amri takatifu za Mwanasheria Kiongozi".

IRGC ni kikosi cha jeshi chenye jukumu la kulinda na kuhifadhi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na lina ushawishi katika masuala yote kuanzia usalama hadi uchumi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI